Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumzia
katika kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Ufugaji na Mipango miji.
Wataalamu
wa Kilimo, Mifugo na Mipango Miji katika Halmashauri ya Itigi na
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakimsikiliza kwa makini Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao Cha kazicha namna ya kuboresha kilimo, Ufugaji na Mipango Miji.
Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumzia
katika kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Ufugaji na Mipango miji.
Wataalamu wa Kilimo, Mifugo na Mipango Miji katika Halmashauri ya Itigi na Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakimsikiliza kwa makini Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao Cha kazicha namna ya kuboresha kilimo, Ufugaji na Mipango Miji.
Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumzia
katika kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Ufugaji na Mipango miji.
Na Mathias Canal,
Singida
Wataalamu wa
Kilimo wametakiwa kuwaunganisha wakulima na Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB) kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa Masoko ili kuongeza
Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo.
Akizungumzia
katika kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Ufugaji na Mipango miji Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa pamoja na wananchi kujituma katika
uzalishaji wa mazao ya chakula na kilimo lakini changamoto Ni kubwa ya namna ya
kuongeza ufanisi katika masoko.
Alisema kuwa
endapo wakulima wataunganishwa na Benki ya Kilimo itakuwa Ni njia pekee ya
kuchagiza na kusaidia kuwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu
kwenda kilimo cha kibiashara ili kukuza uchumi na kupunguza umasikini.
Alisema kuwa
Katika kutekeleza majukumu ya wananchi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
imeanza huduma zake kwa kulenga minyororo michache ya ongezeko la thamani
katika kilimo ambapo mikopo ya aina mbalimbali hutolewa kuwezesha wakulima
kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini Tanzania.
Katika kikao hicho
Cha kuwakumbusha majukumu wataalamu hao Mhe Mtaturu amewataka kuandaa mpango
kazi wa mazao ya Kilimo hususani mazao ya chakula na Biashara.
"Ili kuwe na
kilimo kizuri na tija kwa wananchi, Wataalamu mnapaswa kuzingatia uwepo wa
Pembejeo za kilimo na mbegu Bora za kisasa ambazo zinazalisha mazao mengi"
"Tufanye hivi
ili kuwa mfano Bora katika Mnyororo wa thamani ambao Ni sera ya Taifa ya
viwanda kuchakata mazao ili kuondoa uuzaji wa malughafi na hivyo kuuza
bidhaa" Alisema Mhe Mtaturu
Aliongeza kuwa
kupitia Mnyororo wa thamani utapandisha thamani ya Mazao ya Wakulima ikiwa ni
pamoja na kujiunga kwenye vyama vya Ushirika Jambo ambalo litaibua chachu ya
wananchi kutilia mkazo zaidi katika kujiusisha na kilimo.
Mhe Mtaturu
Alimuelekeza Katibu Tawala wa Wilaya ya Manyoni kuandaa kikao na maafisa ugani
ili kukumbushana ufanisi na namna Bora ya kuendeleza Kilimo kwa wananchi kuanza
kulima mazao ya kipaombele yaliyoelekezwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa
ambayo Ni zao la Pamba, Korosho, Chai, Kahawa na Tumbaku.
Alisema pomoja na
mazao ya kipaombele pia wananchi wanapaswa kuendelea kuongeza nguvu katika
mazao yanayostawi kwa wingi Wilayani humo ikiwa Ni pamoja na zao la Alizeti na
zao la Dengu.
Katika upande
mwingine Mhe Mtaturu alishauri wataalamu wa Mifugo kutilia msisitizo Ufugaji wa
kisasa (Ziro Grazing) kwa kutembelea na kupata utaalamu wa Ufugaji na mbegu
Bora za ya Ng'ombe wa kisasa kwa wataalamu katika Rachi ya Taifa ya Kongwa
(NARCO) na LITI iliyopo Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Naye Afisa Kilimo
Umwagiliaji na Ushirika katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg Chimsala
Fadhili na Afisa Kilimo Umwagiliaji na ushiriki wa Halmashauri ya Itigi Ndg
Renatus Mtatina walimpongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kutangaza kufanya uzinduzi
wa msimu wa Kilimo Wilaya kwani utaongeza chachu na Hamasa kwa wananchi kulima
kwa wingi na tija.
Walisema kuwa
miongoni mwa mambo Msingi na yenye tija katika Jamii Ni pamoja na viongozi kuwa
wabunifu katika utendaji Jambo ambalo llimeonekana kwa Mkuu huyo wa Wilaya.
Uzinduzi wa msimu
wa Kilimo Wilayani Manyoni utafanyika hivi karibuni ambapo utaambatana na
mashindano ya Kilimo katika kila Kijiji, Kata na Tarafa.
EmoticonEmoticon