NA
SEBERA FUGENCE – AFISA UHUSIANO MWANDAMIZI (WCF), MOROGORO
IMEELEZWA
kuwa waajiri ambao hawajisajii na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi hatua kali
zitachukuliwa dhidi yao.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Mhe. Biswalo Mganga katika mafunzo ya
uelemishaji wa Mawakili wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro,
Lindi na Mtwara yaliyofanyika Mkoani Morogoro jana. (leo)
Mheshimiwa
Mganga alisema
hatua za kisheria
zitachukuliwa kwa waajiri watakaobainika kutenda makosa mengine yakiwemo ya
kutowasilisha michango katika Mfuko kwa wakati.
Alisema
lengo la Serikali ni kuona kila mfanyakazi anayeumia, kuugua ama kufariki
kutokana na kazi anapata mafao yake kama ambavyo imeeekezwa katika Sheria ya
Fidia kwa Wafanyakazi
Sura 263 ikisomwa
pamoja na kanuni zake za mwaka 2016.
“Mafunzo
haya yatatoa fursa kwa Ofisi yangu na Maafisa wengine kueleza uzoefu wao
kuhusu namna ya
kuendesha Mashauri ya
Jinai zikiwemo changamoto wanazokutana nazo na mapendekezo ya utatuzi wa
changamoto hizo hasa pale wanaposhughulikia kesi dhidi ya waajiri wanaokiuka
sheria.
Alisema
Ofisi yake ni mdau muhimu sana katika kuhakikisha kuwa matakwa ya Sheria ya
Fidia kwa Wafanyakazi yanatekelezwa kikamilifu na wale wanaoshindwa kutekeleza
wajibu wao wanachukuliwa hatua stahiki za kisheria.
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF) nchini Bw. Masha
Mshomba alisema
Ofisi ya
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ipo kwa mujibu wa Sheria ya Ibara ya 59B ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na moja kati majukumu
yake ya msingi ni kufungua, kusimamia na
kuendesha mashauri ya jinai katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Alisema
Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ni mdau muhimu sana katika
kuhakikisha malengo ya Mfuko huo yanafikiwa kwani ndio wasimamizi wakuu katika
uendeshaji mashauri ya jinai yakiwemo makosa ya jinai yaliyoainishwa kwenye
Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.
Aliitaja
changomoto inayoikabii Mfuko huo kuwa ni
idadi kubwa ya waajiri ambao hawajajisajili na hawachangii kwenye Mfuko
na kuongeza kuwa changamoto hiyo isipopatiwa suluhisho la haraka itaathiri
uwezo wa Mfuko kulipa fidia kwa
wafanyakazi.
Alisema
hadi kufikia juni 30, 2017 Mfuko umelipa fidia ya kiasi cha Shilingi
613,843,555.64 ikiwa ni gharama za matibabu fidia ya ulemavu wa muda mfupi na
ulemavu wa kudumu.
Kwa
upande wa usajili Bw. Mshomba amesema hadi kufikia juni 30, 2017 mfuko tayari
ulikuwa umesajii waajiri 7,857 ambapo hadi kufikia juni 31, 2017 inakadiriwa
kuwa zaidi ya waajiri
13,918 waliopo
Tanzania Bara hawajasajiiwa kwenye Mfuko.
Mfuko
wa Fidia kwa Wafanyakazi ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iiyoanzishwa chini ya
kifungu cha 5 cha Sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Sura 263 marejeo ya
mwaka 2015 kwa lengo la kushughuikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi wanaoumia
ama kuugua ama kufariki wakati wakitekeeza majukumu ya mwajiri kwa mujibu wa
mikataba ya ajira zao.
Mkurugenzi Mkuu
wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)
Bw. Masha Mshomba akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa
Mashtaka (DPP),
Bw. Biswalo Mganga kwenye Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF) kwa
Mawakii wa Serikali
wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani
Marogoro leo Oktoba 4, 2017.
Baadhi
ya Washiriki wa Mafunzo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mashtaka katika Mafunzo ya
Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa Mawakii wa Serikali wa
Mikoa ya Dar es
Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro
EmoticonEmoticon