NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, MHANDISI RAMO MAKANI AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUTUNDIKA MIZINGA KITAIFA MKOANI SIMIYU

October 04, 2017
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu baada ya kuwasili wilayani hapo kwa ajili ya kuongoza maadhimisho ya siku ya utundikaji wa mizinga kitaifa yaliyofanyika jana mkoani humo.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akitundika mzinga wa kisasa wa nyuki katika Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Jumla ya mizinga 50 ilitundikwa wilayani humo. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ni “Ufugaji nyuki kibiashara unachangia katika ukuaji wa viwanda”.
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa (kulia) akitundika mzinga wa kisasa wa nyuki katika Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Jumla ya mizinga 50 ilitundikwa wilayani humo. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ni “Ufugaji nyuki kibiashara unachangia katika ukuaji wa viwanda”. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akimuelekeza jambo Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa kuhusu upatikanaji wa vifungashio bora vya mazao ya nyuki (asali na nta) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. 
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Nyuki wa TFS Kanda ya Ziwa, Samuel Magire kuhusu kifaa maalum aina ya Analogy Honey Refractometer kinavyopima ubora wa asali kwa kuangalia wingi wa maji na sukari wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ni “Ufugaji nyuki kibiashara unachangia katika ukuaji wa viwanda”. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akipima ubora wa asali kwa kutumia kifaa maalum aina ya Analogy Honey Refractometer  ambacho huangalia wingi wa maji na sukari wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza na Afisa Nyuki wa TFS Kanda ya Magharibi, Karim Solyambi kuhusu ufugaji wa nyuki kwa kutumia mizinga ya kisasa ambayo huongeza uzalishaji wa asali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. 
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akizungumza na Afisa Nyuki wa TFS Kanda ya Ziwa, Samuel Magire kuhusu ufugaji wa nyuki kwa kutumia mizinga ya kisasa ambayo huongeza uzalishaji wa asali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Benson Kilangi.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akiangalia tuzo na cheti walichopewa kikundi cha Isengwa Lagangabilili kwa kuwa wafugaji bora wa nyuki katika Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Benson Kilangi
 Baadhi ya wananchi walioshiriki Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa maadhimisho hayo kutoka kwa mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (hayuko pichani). Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ni “Ufugaji nyuki kibiashara unachangia katika ukuaji wa viwanda”. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani azingumza katika mkutano wa hadhara kwenye maadhimisho hayo katika kijiji cha Lagangabilili wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili akizungumza katika maadhimisho hayo.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Tele Ndaki akiwasilisha salamu za Mkoa kwenye maadhimisho hayo.
Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama (CCM), Serikali, waandaji pamoja na waratibu wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.
Mbunge wa Itilima, Njalu Daudi Silanga akisalimia wananchi kwenye mkutano wa hadhara wakati wa maadhimisho hayo.
Burudani ya kucheza na nyoka pia ilikuwepo katika maadhimisho hayo. 
(PICHA NA HAMZA TEMBA - WIZARA YA MALISILI NA UTALII)
HOTUBA YA NAIBU WAZIRI, MHANDISI RAMO MAKANI KATIKA MAADHIMISHO HAYO
HOTUBA YA MKURUGENZI WA IDARA YA MISITU NA NYUKI, DKT. EZEKIEL MWAKALUKWA KATIKA MAADHIMISHO HAYO

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »