Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi (katikati),akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo.Wengine pichani ni Maofisa Waandamizi wa kampuni hiyo
Kikosi kazi cha timu ya mauzo ya Nyanza Bottlers katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Mchongo chini ya kizibo
Msafara wa magari ya kampuni ya Nyanza Bottlers yakipita mitaani katika mji wa Mwanza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo
Kampuni ya Coca-Cola, imezindua kampeni kubwa ya wiki 10 kwa wateja wake inayojulikana kama ‘Mchongo Chini ya Kizibo’ ambayo itawawezesha wateja wake wa mikoa ya kanda ya ziwa na jirani kujishindia zawadi nono za fedha taslimu zaidi ya milioni 400,bodabado 100,televisheni 60 aina ya SONY LED zenye inchi 32,T-shirts , kofia na soda za bure.
Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi, alisema lengo la promosheni hii ni kuleta msisimko zaidi kwa wateja wanywaji wa soda zote zinazozalishwa na kampuni ya Coca-Cola waliopo mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma, na mikoa mingine jirani ya kanda ya ziwa.
“Kampuni yetu ya Coca-Cola katika kutoa shukrani kwa wateja wetu wanaotuunga mkono tumekuwa tukifanya promosheni mbalimbali zenye lengo la kuleta furaha na kubadilisha maisha yao kupitia Coca-Cola na promosheni ya ‘Mchongo Chini ya Kizibo’ tunayoizindua leo. Kwa kunywa soda aina yoyote inayozalishwa na kampuni ya Coca-Cola wataweza kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu, bodabado, televisheni aina ya SONY LED zenye inchi 32, T-shirts , kofia na soda za bure.” Alisema Kisusi.
Alisema ili mteja kujishindia zawadi atabandua kiambatanisho laini kilichopo chini ya kizibo cha soda. Kwa upande wa fedha taslimu kuna zawadi za shilingi 5,000/-, 10,000/- na 100,000 na zaidi ya shilingi milioni 400/- zimetengwa kwa ajili ya kushindaniwa na wateja, ambapo kwa upande wa zawadi ya bodaboda anachotakiwa kufanya mteja ni kukusanya vizibo vitatu vyenye picha zinazokamilisha picha ya bodaboda – kuonyesha upande wa Nyuma, Katikati na Mbele.
Kisusi aliongeza kuwa pia zawadi nyinginezo za Televisheni, kofia, T-shirt na soda za bure zinapatikana chini ya kiambatanisho laini chini ya kizibo kama zilizvyo zawadi kubwa.
“Natoa wito kwa wateja wetu kuchangamkia promosheni hii ili waendelee kuburudika na soda zinazotengenezwa na kampuni ya Coca-Cola sambamba na kunufaika kwa zawadi za kuleta furaha na kuboresha maisha yao, familia zao na wapendwa wao.”
Kuhusu jinsi ya kupata zawadi alisema kuwa zawadi zote kwa washindi zitatolewa bila urasimu wa aina yoyote kuanzia kwenye maduka ya rejareja, mawakala maalumu wa kusambaza vinywaji vya kampuni ya Coca-Cola na kwenye kiwanda cha Nyanza Bottlers.
Soda za kampuni ya Coca-Cola ambazo zitakuwa na zawadi kwenye ganda la vizibo ni Coca-Cola, Fanta, Sprite, Tangawizi, Sparleta na Novida.
EmoticonEmoticon