KILIMO CHENYE TIJA BILA YA KUWA NA SOKO LA UHAKIKA NI KAZI BURE KWA MKULIMA

August 14, 2017


 Mkuu wa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Selemani Mzee, akizungumza na maofisa ugani wakati akifungua mafunzo ya namna ya kutumia sayansi na teknolojia katika kuboresha kilimo kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi leo ambayo yaliandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB). Kutoka kushoto ni Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa wilaya hiyo, Winfrid Tamba, Mtafiti Bestina Daniel kutoka COSTEC na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wa wilaya hiyo, Kanzumari Malilo.


 Ofisa Tawala wa wilaya hiyo, Benaya Kapinga akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa wilaya hiyo, Selemani Mzee (kushoto) kuzungumza na maofisa ugani. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Masasi, Juma Satmah.
 Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Masasi, Juma Satmah, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
 Watafiti watoa mada wakisubiri kutoa mada zao. Kutoka kulia ni Dk. Nicholaus Nyange, Benadetha Kimata na Dk. Dk.Emmarold Mneney.
 Mshauri wa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Mkoa wa Mtwara, Ally Linjenje, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
 Mtafiti kutoka Costech, Bestina Daniel akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo kwa maofisa ugani.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wa wilaya hiyo, Kanzumari Malilo, akishukuru COSTECH kwa kuwapelekea mafunzo maofisa ugani wa wilaya hiyo.
 Maofisa ugani wakiwa kwenye mafunzo hayo.
 Mafunzo yakiendelea.
 Mwenzeshaji wa mafunzo hayo Kutoka OFAB Dk.Emmarold Mneney, akitoa mada.
 Muonekano wa chumba cha mafunzo hayo.
 Viongozi wa Wilaya hiyo wakiwa kwenye mafunzo hayo.
 Ofisa Ugani, Saidi Mnangona kutoka Kata ya Chigugu, akiuliza swali.
 Ofisa Ugani, Jacob Mbuya kutoka Kata ya Chikunja, akiuliza swali

Ofisa Kilimo, Lothi Philipo Mollel kutoka Kata ya Chiungutwa, akiuliza swali.
Mtafiti wa Mazao ya Mizizi na Jamii ya Viazi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mtwara Naliendele, Benadetha Kimata, akitoa mada
Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa matumizi ya kilimo, Dk.Nicholaus Nyange, akitoa mada.

Na Dotto Mwaibale, Masasi

MKUU  wa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Selemani Mzee amesema kilimo chenye tija kitakuwa na maana iwapo kutakuwa na masoko ya uhakika ya kuuza mazao  kinyume ya hapo itakuwa kazi bure kwa wakulima.

Hayo ameyasema wilayani hapa leo  wakati akifungua mafunzo ya namna ya kutumia sayansi na teknolojia katika kuboresha kilimo kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi ambayo yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB). 

Mzee alisema bila ya kuwa na masoko ya kununua mazao ya wakulima itakuwa ni kazi bure hivyo ni vema kilimo chenye tija kikaenda sanjari na kupatikana kwa masoko hayo.

Mzee alisema wakulima wa Masasi wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kulima kwa kutumia nguvu nyingi lakini anavuna kidogo pamoja na matatizo ya masoko. Alisema teknolojia ya kilimo ndio itakayomkomboa kwani atalima eneo dogo na kuvuna mazao mengi.

Katika hatua nyingine Mzee aliwataka maofisa ugani wilayani mwake kuhakikisha  wanawasaidia wakulima kulima mahindi ya  WEMA ambayo yanahamasishwa na watafiti wa masuala ya kilimo kutokana na kustahimili ukame.

“Ninachowaomba tujipange kuwasaidia wakulima wetu namna ya kupata masoko ya mazao yao, watatumia teknolojia je wakishapata mazao mengi watauza wapi? Lakini pia tuwasaidie akishavuna mazao yake atahifadhi vipi? alihoji Mzee.

Alisema kwamba mbinu za kilimo cha teknolojia ambayo inahamaishwa na wanasayansi kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ndio tiba pekee ya kuachana na kilimo kisicho na tija.

“Nawaagiza kwamba mkitoka hapa, mkawahamasishe wakulima wenu angalau walime hata nusu ekari ya mahindi haya yanayohamasishwa kutumiwa na watafiti wetu. Nafahamu kwamba wakipata mazao mengi lazima msimu ujao wataongeza eneo la kulima,” alisema Mzee.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka pia maofisa ugani hao kuhakikisha kwamba licha ya kulima mazao hayo, lakini pia wakahamasishe wakulima kutumia mbegu za mihogo hasa kiroba ambayo inahamasishwa na watafiti wa Kituo cha Utafiti Naliendele Mtwara.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Masasi, Juma Satmah alisema kuwa kundi hilo la wataalam wa kilimo ni muhimu sana kwa maendeleo ya wilaya hiyo kwa kuwa ndio wahamasishaji wakubwa wa kilimo ingawa mara nyingi limekuwa likisahaulika.


Mwenzeshaji wa mafunzo hayo kutoka Kutoka OFAB Dk.Emmarold Mneney aliwaambia washirikiwa mafunzo hayo kuwa bioteknolojia katika kilimo itasaidia kuepukana na magonjwa, wadudu waharibifu na pia inasaidia mazao kukabiliana na ukame.

Alisema kuna teknolojia ya uzalishaji wa mbegu kwa kutumia tishu ambayo kwa sasa imesaidia kupata mbegu nzuri za muhogo, korosho na nanasi na kudhibiti wadudu waharibifu kama  mahindi ambazo zinajulikana kama WEMA.

Alisema teknolojia nyingine ambayo imebuniwa na watafiti ni kupata mbegu kwa njia ya uhandisi jeni (GMO). Alisema kwa sasa watafiti wanaendelea kufanya utafiti wa mihogo na mahindi ili waangalie ukanzani wa mazao hayo dhidi ya magonjwa, ukame na uharibifu wa wadudu.

Mtafiti Bestina Daniel kutoka COSTECH alisema kupitia Jukwaa la bioteknolojia kwa maendeleo ya kilimo nchini wameona waendeshe mafunzo kwa wakagani ambao ndio nguzo ya kilimo ili  kuwakumbusha majukumu yao na kuwapatia  mbinu malimbali za kilimo kwa kuwa wanategemewa na wakulima. 

Aidha aliongeza kuwa mafunzo hayo ya siku moja kwa maofisa  ugani hao yamelenga kuwapatia mbinu bora za uzalishaji wa mazao ya korosho, mahindi na Mihogo na nafasi ya matumizi ya bioteknolojia katika kusaidia kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima na kuongeza uzalishaji.

Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Philbert Nyinondi kwa nyakati tofauti aliwajulisha washiriki wa mafunzo hayo kuwa wakulima wa Tanzania hawajabahatika kulima zao lolote lililofanyiwa uhandisi jeni.

" Hadi sasa, hakuna mkulima wa Tanzania aliyewahi au anayelima mazao ya Uhandisi jeni (GMO), na sio kulima tu hata wale wanaofuga, hakuna mfugaji mwenye mnyama wa GMO Tanzania." alisema Nyinondi.

Akifafanua kauli yake Philbert Nyinondi alisema watu wengi kwa kutofahamu au kwa makusudi wanawachanganya wakulima hasa wale wanaotumia mbegu za chotara na kuwaambia ndo GMO.


"Tumefikia upotoshaji wa kiwango cha juu sana kwenye jamii. Mtu akiona kitu bora au kilichoboreshwa mfano maembe makubwa, mananasi makubwa, mimea inayokuwa kwa muda mfupi na hata kuku wa kisasa huitwa GMO. Ukweli ni kwamba labda Serikali yetu iamua wakulima wa Tanzania wafaidi teknolojia hii mapema zaidi. Vinginevo, kwa kasi ya watafiti wetu, tunaweza kuwa na zao la kwanza la GMO kwa mkulima kuanzia mwaka 2022" alisema Nyinondi.  


Alitanabaisha kuwa upatikanaji wa mazao GMO hata hiyo mwaka 2022  utategemea matokeo ya utafiti unaendelea nchini, tathimini zitakazofanywa na Taasisi ya serikali kama kamati ya kusimamia matumizi salama ya bioteknolojia NBC, 


Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Mamlaka wa Uthibiti wa Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na wepesi wa kampuni za mbegu zenye usajili Tanzani kuzalisha mbegu za kutosha kwa ajili ya kusambaza kwa wakulima.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »