WAZIRI LUKUVI AZINDUA SAFARI CITY ARUSHA

August 14, 2017
Na. Hassan Mabuye

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amezindua ujenzi wa Mji wa Safari pamoja na kuwapa hati wakazi 100 wa mji wa Arusha.

Safari City ni mji wa kisasa uliopangwa vizuri kwa kufuata sheria na kanuni za mipango miji uliopo Jijini Arusha.Eneo hili limepangwa viwanja vya nyumba za makazi, ofisi, biashara, hoteli, shule na viwanda vidogo vidogo. 

Viwanja hivi vina huduma zote muhimu kama vile miundombinu ya maji, umeme, barabara na mfumo wa maji taka.Mauzo ya viwanja hivi yanakwenda sambamba na mauzo ya nyumba za mfano ambapo viwanja vya makazi vinaanzia Tsh 7M na kuendelea.

Katika ziara hii Waziri Lukuvi alipokea taarifa ya ufutwaji wa mashamba kumi na mbili (12) yaliyoko Halmashauri ya Meru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Baada ya kupokea taarifa hiyo Mhe. Lukuvi alitembelea eneo la Ekari mia moja (100) lililopimwa viwanja kwa ajili ya utatuzi wa viwanja mbadala kwa Halmashauri ya jiji la Arusha.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikata utepe wakati wa uzinduzi wa nyumba za mfano ambazo kati ya nyumba 10 zilizojengwa na NHC, nyumba saba zimeishanunuliwa. 
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikabidhi hati kwa wamiliki wa awali wa eneo la Safari City wakati wa uzinduzi wa nyumba za mfano na makabiadhiano ya Hati Miliki za Viwanja 100 kwa ajili ya Uendelezaji.

  Baadhi ya Nyumba zilizokamilika ujenzi wake katika Eneo la Safari City mkoani Arusha.
 Waziri Lukuvi akipokea taarifa ya ufutwaji wa mashamba kumi na mbili (12) yaliyoko Halmashauri ya Meru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
 Waziri Lukuvi pamoja na viongozi wa mkoa wa Arusha wakifanya ukaguzi wa eneo la Ekari mia moja (100) lililopimwa viwanja kwa ajili ya utatuzi wa viwanja mbadala kwa Halmashauri ya jiji la Arusha.

 Waziri Lukuvi pamoja na viongozi wa mkoa wa Arusha wakifanya ukaguzi wa eneo la Ekari mia moja (100) lililopimwa viwanja kwa ajili ya utatuzi wa viwanja mbadala kwa Halmashauri ya jiji la Arusha. 
  Eneo la Ekari mia moja (100) lililopimwa viwanja kwa ajili ya utatuzi wa viwanja mbadala kwa Halmashauri ya jiji la Arusha.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi Mkuu wa Mkoa Arusha Mrisho Gambo na Mkuu wa Wilaya Arusha Gabriel Fabian wakiteta jambo wakati wa Uzinduzi wa Safari City.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »