Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Mhe. Luhaga Mpina akitia sahihi katika kitabu cha wageni katika Ofisi za Makao
Makuu ya jeshi la Police kisiwani Zanzibar, Mpina yupo kisiwani humo katika
ziara ya kutembelea baaadhi ya maeno ya Muungano, kulia ni kaimu kamishna wa
jeshi la Police Zanzibar kamanda Juma Yusuph Ali.
Katika picha baadhi ya Makamishna wa Jeshi la Police katika
Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo kisiwani Zanzibar wakimsikiliza Naibu Waziri Mpina, ambaye hayupo pichani alipokuwa
akizungumza nao.
Katika picha, Naibu Waziri Mpina akishikilia moja ya
Jalada la miaka ya nyuma la maombi ya hati ya kusafiria huku akiuliza swali
katika maktaba ya Jeshi la Uhamiaji
katika Ofisi ya Makao makuu ya jeshi hilo kisiwani Zanzibar
Naibu Waziri Mpina katika Picha ya Pamoja na viongozi wa
Jeshi la Uhamiaji kisiwani Zanzibar na maafisa wa Idara ya Muungano kutoka
Ofisi ya Makamu wa Rais, baada ya kumaliza ziara yake katika Ofisi hizo .
Kulia Naibu Waziri Mpina akijibu swali la mwakilishi wa ITV
na Radio one Zanzibar Farour Kareem (kushoto) kwa niaba ya waandishi wa
habari hawapo pichani, katikati ni Kamishna wa Jeshi la Uhamiaji Zanzibar Bw. Johari Masoud Sururu.
NA EVELYN MKOKOI
Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina amefanya ziara katika
baadhi ya taasisi za Muungano kisiwani Zanzibar.
Katika ziara yake alipotembelea
ofisi za jeshi la Uhamiaji kisiwani humo Mpina alisema kuwa, Taasisi za
Uhamiaji na jeshi la Police ni muhimu sana katika ustawi wa muungano wa Tanzania
Bara na Visiwani kwani Muungano huu unategemea sana amani, na hauwezi kuwepo
muungano kama kuna vurugu na uvamizi wa wahamiaji haramu.
Alisisitiza kuwa ni lazima
taasisi hizo kutembelewa na kuziona mara kwa mara namna zinavyofanya kazi na
kuona changamoo zao ili serikali iweze kuzifanyia kazi na kuwawezesha waweze
kufanikisha majukumu yao vizuri na katika usimamizi wa sheria kwa ujumla wake.
“ Nataka niseme dhahiri
kuwa taasisi hizi zinautendea haki Muungano kutokana na wao wenyewe wanavyotimiza
majukukumu yao pamoja na changamoto zinazowakabili na kuiweka nchi katika
utulivu na usalama.” Alisisitiza Mpina.
Naibu Waziri Mpina
aliongeza kwa kusema kuwa “ nimeona jinsi ambavyo wanasimamia na kutekeleza majukumu
yao nimeona namna ambavyo wanatoa vibali vya kusafiria, nimeelezwa kwamba kwa
siku moja wastani wa maombi ya vibali vya kusafiria ni kati ya maombi 80 mpaka
120 lakini wao wana uwezo wa kutoa vibali zaidi ya 150 kwa siku hiyo ni zaidi
ya maombi yanayotolewa na wanatoa vibali hapa hapa zanzibar haya nimafanikio
makubwa katika Muungano wetu”. Alisema
Kwa upande wake kaimu
kamishna wa jeshi la Police Zanzibar kamanda Juma Yusuph Ali, alisema ili
kukabiliana na changamoto za kiusalama kisiwani humo kunahitajika juhudi na
ushirikino wa pamoja kati ya wananchi jamii na wadau . Alitoa wito kwa jamii
kushirikiana na jeshi la Police ili kuweza kuzitatua Chngamoto hizo.
Katika ziara yake kisiwani
Zanzibar Naibu Waziri Mpina alitembelea Ofisi za uhamiaji, Jeshi la Police na
Ofisi za wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Africa mashariki.
EmoticonEmoticon