Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Anna Abdallah (katikati) akiwa na Girl Guides waliorejea nchini kutoka kwenye programu ya Yess ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya uongozi, utamaduni na maadili katika nchi za Uganda, Madagascar, Zimbabwe na Zambia. Hapo ilikuwa wakati wa hafla maalumu iliyoandaliwa na TGGA Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapongeza na kupata mrejesho wa walichojifunza walipokuwa kwenye programu hiyo inayodhaminiwa na Norwey.Anna Abdallah aliwapongeza wasichana hao wanne kwa kuiwakilisha vizuri TGGA na Tanzania katika programu hiyo nje ya nchi.
Kutoka kulia ni Ummy Mwabondo alikwenda Zambia, Farida Mjoge aliyekuwa Uganda, Elizabeth Betha (Madagascar) na Edna Chembele (Zimbabwe),
Girl Guides hao wakipata msosi wakati wahafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa kwa ajili yao kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Oysterbay, Dar es Salaam.
Anna Abdallah akiotoa nasaha na pongezi kwa Girl Guides kwa kuiwakilisha vizuri TGGA NA Tganzania kwa ujumla, ambapo aliwataka watumie mafunzo waliyoyapata kwa kutoa mafunzo kwa wasichana wenzao nchini.
Wakiwa na furahani Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi (kushoto), Anna Abdallah (katikati) na Mjumbe wa TGGA, Agnes Makenya
Katibu Mkuu wa TGGA Tanzania, Grace Shaba akitoa neno la ukaribisho muda mfupi kabla ya Girl Guides waliorejea nchini kutoka nje ya nchi kwenye programu hiyo kuelezea mambo mbalimbali waliyoyafanya na kujifunza
Grace Shaba akiwatambulisha Girl Guides hao
i Ummy Mwabondo akielezea kwa njia ya picha kazi mbalimbali alizokuwa anazifanya alipokuwa Zambia
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya TGGA, Sophia Mjema akitoa ufafanuzi wakati Girl Guides wakielezea mafanikio na changamoto ya mafunzo yao nje ya nchi
Girl Guides Farida akielezea mambo mbalimbali aliyoyafanya akiwa Uganda kwa muda wa miezi sita.
Viongozi na wageni waalikwa wakionesha ishara ya TGGA
Viongozi wa Girl Guides Makao Makuu ya TGGA wakiwa na furaha wakati wa hafla hiyo
Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi (kushoto), akiwa na Kamishna wa Kimataifa wa TGGA wakijadili jambo
Sasa ni wakati wa msosi
Mwenyekiti wa TGGA, Profesa Martha Qorro akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya TGGA, Anna Abdala kuzungumza katika hafla hiyo.
Mwakilishi wa wazazi wa Girl Guides hao, Florence Gondwe akitoa shukrani kwa TGGA kwa kuwapatia wasichana hao fursa ya kwenda nje ya nchi kwenye programu hiyo ambayo alidai itawasaidia sana kimaisha.
Kamishna Hangi akitoa neno la shukrani kwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo pamoja na Girl Guides
Wakiwa katika picha ya pamoja
Anna Abdallah akiagana na Girl Guides baada ya hafla kumalizika
EmoticonEmoticon