Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo linapojengwa jengo la Wazee Kolandoto. ambapo aliwela jiwe la Msingi la jengo la makazi ya Wazee Kolandoto.
Na Mwandishi Wetu Shinyanga
Naibu Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla amesema
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), itaendelea
kusimamia haki za wananchi wake kuanzia watoto, Vijana na Wazee ilikulinda haki
na hutu wao hapa nchini.
Dk.
Kigwangalla amesema hayo Julai 22,2017, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika
shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bweni la makazi ya Wazee ya
Kolandoto, yaliyopo umbali wa zaidi ya
KM 10, kutoka Shinyanga Mjini, mkoani Shinyanga.
Ambapo mabli na kuweka jiwe hilo la msingi la
ujenzi wa bweni hilo, pia alifungua rasmi jiko maalum la gesi ambalo litakuwa
likitumika kwa ajili ya chakula cha wazee hao pamoja na kukabidhi Bajaji ya
miguu mitatu itakayorahisisha usafiri kwa wazee hao kwenye makazi yao hayo.
Makazi ya
wazee ya Kolandoto ni ya muda mrefu, ambapo kwa uanzishwaji wa ujenzi wa bweni
hilo litakuwa faraja kwa wazee wanaoishi hapo kwani litakuwa na uwezo wa
kuchukua wazee zaidi ya 20.
“Serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania imeweka msisitizo kuendelea kuwaenzi wazee kwa michango
yao katika kulijenga taifa letu. Serikali ina jukumu la kuwatambua wazee na
kuwapatia huduma za matibabu bila malipo na kuhakikisha wanalindwa dhidi ya
vitendo vya ukatili ikiwemo mauaji. Katika kutekeleza haya, Serikali ya Awamu
ya tano imeunda Wizara inayosimamia masuala ya wazee ili kuhakikisha haki zao
zinalindwa. Katika kufanikisha azma
hiyo, serikali inahudumia makazi hayo 17 ya
wazee wasiojiweza hapa nchini” alieleza Dk. Kigwangalla
Mpaka
likikamilika litatosha kuwahudumia wazee wasiojiweza 20. Hivi sasa kuna wazee
16, kituoni hapa. Majengo ya zamani ni ya udongo na yamekaa zaidi ya miaka 50
bila ukarabati.
Kimsingi
hayafai tena kwa matumizi ya binadamu (yapo condemned). Tumeyakarabati ili
yaweze kutumika wakati tukijenga jengo hili jipya la kisasa” alieleza Dk.
Kigwangalla.
Dk.
Kigwangalla aliongeza kuwa, Pamoja na ujenzi wa jengo hilo kwenye makazi ya
wazee wasiojiweza, Wizara yake imefanya maboresho makubwa na muhimu sana kwenye
makazi hayo ikiwemo kuweka majiko ya kisasa ya gesi, vyombo vya kupikia na
kulia chakula, huduma ya maji, vifaa vya huduma ya kwanza, vifaa vya chumba cha
kulala na vyombo vya usafiri (Bajaj)na huduma muhimu kwa wazee hao.
Hata hivyo,
Dk. Kigwangalla ameeleza pamoja na ufinyu wa bajeti wanayopewa kwa ajili ya idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii,
amewapongeza wataalamu wa idara hiyo wakiongozwa na Katibu Mkuu, Ndg. Sihaba
Nkinga, kwa ubunifu uliowezesha kufanyika bila kupokea pesa ya kutekeleza
miradi ya maendeleo.
“Wataalamu
wanapaswa kutumia ujuzi wao kuleta tija na ufanisi kwenye utekelezaji wa
majukumu tuliyopewa. Nawapongeza sana kwa kufanya jambo hili kubwa na la
umuhimu” alimalizia Dk. Kigwnagalla.
Hata hivyo,
Dk. Kigwangalla amesema kuwa, Serikali itaendelea kuimalisha makazi ya wazee
hao kwani inatambua thamani yao hivyo ni jukumu la kuwasaidia huku pia akitoa
rai kwa Jamii kuweza kukaa nao wazee hao kwani Uzee unapitiwa na jamii yote na
haukwepi.
Kwa Mujibu
wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka
2012, Tanzania inakadiriwa kuwa na Wazee
2,507,568 (Wanawake 1,307,358, Wanaume
1,200,210) sawa na asilimia 5.6 ya wananchi wote. Aidha, kwa mujibu wa Sensa
hiyo idadi hiyo inakadiriwa kuongezeka hadi kufikia wazee 2,777,002 (wanawake
1,447,659, wanaume 1,329,343) ifikapo Disemba, 2017.
Ongezeko
hili la idadi ya wazee ni kiashiria cha kuendelea kuimarika kwa hali ya
upatikanaji wa huduma za msingi kwa jamii ikiwemo huduma ya
afya upatikanaji wa chakula na
huduma bora za matibabu; hivyo kuchangia kuongezeka kwa umri
wa kuishi.
Hadi sasa Serikali
Serikali inahudumia makazi 17 ya wazee
wasiojiweza na ambao hawana ndugu na jamaa
ikiwemo kituo hicho cha Kolandoto, Mkoani Shinyanga.
Andrew Chale
Blogger
Personality | Journalist | Activist | Online Editor dewjiblog |
Comedian |Volunteer Red Cross | Sauti za Busara & ZIFF Festivals
2007 to present.
Email: andrewchale@gmail.com
Telephone: +255222122830 Fax: +255222126833
Golden Jubilee Towers, Ohio Street,20th Floor
Po Box 20660, Dar es Salaam,Tanzania
EmoticonEmoticon