Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa
Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafsi wa wilaya ya
Mbozi kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Vwawa wilayani
Mbozi Julai 23, 2017. Kulia ni mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Songwe, Chiku Galawa Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa
Limdi, Erasto Zambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Cashier wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Bahati Chomoka pia amesimamishwa.kazi.
DT wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Simon Noeli ambaye pia amesimamishwa kazi.
DED wa Mbozi, Elisey Mgoyi mmoja
wa watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi ambao Waziri Mkuu
aliagiza wasimashwe kazi na wafanyiwe uchunguzi na TAKUKIURU.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua ujenzi wa jengo la Mkuu wa Mkoa wa Songwe nje kidogo ya mji wa
Vwawa mkoani Songwe Julai 23, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe,
Chiku Galawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
mkewe Mary (kulia kwake) wakitazama Kimondo wakati walipotembelea Kituo
cha Mambo ya Kale cha Mbozi mkoani Songwe Julai 23, 2017.(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
mkewe Mary wakiwapungia wananchi wa wilaya ya Mbozi wakati walipowasili
kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kyalele wilayani humo kuhutubia
mkutano wa hadhara, Julai 23, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe,
Chiku Galawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
mkewe Mary wakitazama nguo za batiki wakati walipotembelea banda la
wanawake wajasiriamali wa Mbozi kabla ya mkutano wa hadahara
uliohutubia wa Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya
Nalyelye wilayani Mbozi, Februari 23, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Songwe, Chiku Galawa. (Picha na Ofisi a Waziri Mkuu)
……………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi
mkoani Songwe, Bw. Eliseyi Mgoyi pamoja na maofisa wengine watatu kwa
tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma.
Pia amemuagiza Kamanda wa Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Songwe, Bw. Damian
Sutta kuwakamata na kuanza kuwachunguza haraka maofisa hao na kisha
ampelekee taarifa ofisini kwake.
Waziri Mkuu amewasimamisha kazi
maofisa hao leo (Jumapili, Julai 23, 2017) wakati alipozungumza na
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwenye ukumbi wa Shule ya
Sekondari Vwawa, akiwa katika ziara yake ya kikazi.
Maofisa wengine waliosimamishwa
kazi ni pamoja na Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo Bw. Simon Noel, Bw.
Bahati Chomoka ambaye ni Cashier na Bw. Remmy Haule ambaye ni Ofisa
Ugavi.
Waziri Mkuu amesema Maofisa hao
wamekiuka sheria za matengenezo ya magari ya Serikali kwa kwenda
kutengeneza katika gereji ambazo hazikusajiliwa na wala hazifanyi
shughuli hiyo, jambo ambalo halikubaliki.
Amesema Kampuni ya Umbwila ni
moja kati ya Kampuni zinazolipwa fedha nyingi za utengenezaji wa magari
ya Halmashauri ya wilaya ya Mbozi huku ikiwa haina sifa za kufanya kazi
hiyo ya utengenezaji magari.Kampuni zingine ni Julius Diesel, Kasaba na
Mtoni Garage.
“Mfano duka la Umbwila ambalo
linauza vipuri vya magari lakini Halmashauri inalilipa fedha kwa ajili
ya utengenezaji wa magari jambo ambalo si sahihi kwa sababu lile ni duka
la vipuri na si gereji. Wanamlipa muuza vipuri kama mtengeneza magari”
Waziri Mkuu ameongeza kuwa
“hatuwezi kuendesha Serikali kwa namna ambayo haikubaliki kwani watu
tuliowapa dhamana ndio wanaongoza kwa vitendo vya rushwa na ufisadi.
Wameifanya Halmashauri hii kama shamba la bibi.”
Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu
amemtaka Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mheshimiwa Eric Ambakisye
kuhakikisha anasimamia vizuri utendaji ndani ya Halmashauri hiyo na
kwamba Serikali inataka watu waadilifu na wenye uaminifu na nidhamu.
“Halmashauri inanuka rushwa
tunataka iwe safi. Hatuwezi kukubali kuona Halmashauri hii na zingine
nchini zikigeuzwa kuwa magenge. Kwa Serikali hii no, hatuhitaji rushwa
wala harufu ya ufisadi.”
Waziri Mkuu amesema Serikali
haiwezi kuvumilia kuona watumishi waliopewa dhamana wakijinufaisha kwa
fedha za umma na kuwaacha wananchi wakiendelea kuteseka kwa kukosa
huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo za maji, afya na elimu, hivyo
itaendelea kuwachukulia hatua.
Pia Waziri Mkuu amewataka
Madiwani na Wakuu wa Idara katika Halmashauri zote nchini wabadilike na
wahakikisha wanashirikiana na kufanya kazi kwa ushirikiano kwani
wakigawanyika watashindwa kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia
wananchi.
EmoticonEmoticon