UBALOZI WA JAPAN NCHINI WAAHIDI KUENDELEA KUSAIDIA MIRADI MBALIMBALI YA KIMAENDELEO MKOANI IRINGA

July 23, 2017
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida na Waziri Lukuvi wa pili kulia na wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ,mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakishiriki kukata utepe kuzindua bweni Shule ya Idodi sekondari leo
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida na Waziri Lukuvi wa pili kulia na wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ,mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakishiriki kukata utepe kuzindua bweni Shule ya Idodi sekondari leo 
Vitanda vilivyopo katika bweni hilo 
Hili ndilo bweni la kisasa lililojengwa na ubalozi wa Japan nchini 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akimkaribisha balozi wa Japan nchini 
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida akizungumza na wananchi na wanafunzi wa sekondari ya Idodi 
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida akikabidhi taa za mionzi ya jua kwa mkuu wa shule ya sekondari Idodi kulia kwake ni mbunge wa Isiman Wiliam Lukuvi na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na katibu wa CCM Iringa vijijini Dodo Sambo 
Balozi wa Japan nchini akimkabidhi taa hizo mbunge wa Isimani wiliam Lukuvi 
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi ambae ni mbunge wa Ismani akimsaidia balozi wa Japan nchini kukaa katika kiti cha asili ya Kihehe baada ya kuvishwa nguo hizo za heshima 
Balozi wa Japan nchini akivishwa nguo za kichifu wa wahehe 
Balozi wa Japan Masaharu Yoshida akivishwa nguo za kichifu 
balozi wa japan nchini akiwa na nguo za kijadi za kihehe akisema hapa KAZI TU 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kushoto na waziri Lukuvi na DC Iringa Kasesela wakiwa na balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida 
Mbunge wa Ismani na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi akimpongeza balozi wa Japan kwa msaada wa ujenzi wa Bweni 
NA MatukiodaimaBlog 

UBALOZI wa Japan nchini Tanzania umeahidi kuendelea kusaidia miradi mbali mbali ya kimaendeleo ndani ya mkoa wa Iringa na maeneno mengine hapa nchini ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli. 

ubalozi huo wa Japan ambao umesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa Mkoani Iringa kwa kiasi cha shilingi milioni 270.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa Bweni hilo la wanafunzi shule ya sekondari ya Idodi Iringa balozi Masaharu Yoshida alisema kuwa misaada hiyo inatolewa kupitia kodi za watu wa Japan kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za kimaendeleo nchini Tanzania. 

Alisema kuwa hatua Japan kufika kusaidia ujenzi wa bweni hilo katika shule ya sekondari Idodi umetokana na maombi ya mbunge wa Jimbo hilo la Ismani Wiliam Lukuvi ambaye ni waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi aliloomba katika ofisi ya ubalozi kufuatia bweni la awali kuteketea kwa Moto.

"waziri Lukuvi lileta maombi ya mradi wa kujengewa miradi hiyo ya maendeleo ambayo ni Hostel ya wasichana shale ya wasichana Ismani ambayo ilijengwa toka mwaka 2005 na mwaka2008 kujenga jengo la OPD na wodi ya wagonjwa katika zahanati ya Mlowa na mwaka 2010 kununua gari la wagonjwa katika zahanati ya Mlowa... namshukuru Waziri Lukuvi kwa kusimamia vema miradi hiyo"

Balozi huyo alisema kuwa mkataba wa ujenzi wa bweni hilo la wanafunzi Idodi sekondari ulisainiwa February mwaka 2016 kwa dolla za kimarekani 130,166 sawa na milioni 270 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo. 

" Leo nimefurahi kuona ujenzi umekamilika kwa kiwango kizuri vitanda vya kutosha, mfumo wa kuhifadhi maji, Hosteli hii sasa inauwezo wa kulaza wanafunzi 208 kama kusudio la ujenzi ni matumaini yangu mradi huu utatunzwa vema"

Balozi huyo alisema kutokana na usimamizi mzuri walioufanya kampuni ya Koyo Corporation kampuni ya kijapani imetoa msaada wa taa zinazotumia nguvu ya mionzi ya jua kwa ajili ya kutumia wanafunzi wote watakaoishi katika bweni hilo. 

Hata hivyo alisema ubalozi wa Japan nchini utaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania chini ya kauli mbiu ya hapa kazi tu.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza awali akimkaribisha balozi huyo alisema kuwa serikali ya mkoa inafurahishwa na msaada huo ambao umesaidia kupunguza msongamano ya wanafunzi bwenini na hivyo bweni hilo ambalo litatunzwa vizuri. 

Mbunge wa Ismani waziri Lukuvi pamoja na kupongeza msaada huo wa kujengewa bweni na miradi mingine bado amepongeza kwa hatua ya balozi huyu kubariki zaidi ya shilingi milioni 11 zilizobaki katika ujenzi wa bweni hilo kutumika kununua vifaa vya kusambaza maji ya kisima kitakachochimbwa shuleni hapo. 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »