TFF YAMPONGEZA TENGA
Kaimu
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace John Karia
amempongeza Leodegar Chilla Tenga - Rais wa Heshima wa TFF kwa kuteuliwa
kuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Leodegar
Chilla Tenga aliteuliwa Ijumaa iliyopita katika Mkutano Mkuu wa CAF
uliofanyika mjini Rabat nchini Morocco ambako katika kamati hiyo muhimu,
Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zambia (FAZ), Kalusha
Bwalya.
“Hii
ni sifa kwa nchi. Na ni sifa kwa Mheshimiwa Tenga. Tunajisikia fahari
Tanzania kung’ara katika medani za uteuzi katika vyombo vya kimataifa
kama CAF. Uteuzi wake ni kwamba anafungua njia kwa nchi na wengine ili
kufanya vema,” anasema.
Karia
amesema ana imani na Tenga na Bwalya katika kamati yao kwa sababu ni
wachezaji na manahodha wa zamani wa timu za taifa. Itakumbukwa kwamba
Tenga alikuwa akicheza kama mlinzi Bwalya alikuwa mshambuliaji. “Wote ni
wataalamu. wanajua, tutafanikiwa.”
Katika
mkutano huo mbali na kuteua akina Tenga na kuunda kamati nyingine, pia
ulifanya marekebisho ya muundo wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON) na sasa yatakuwa yakifanyika katikati ya mwaka badala ya
mwanzoni mwa mwaka.
Kwa
miaka ya nyuma hadi mwaka huu ambako michuano hiyo ilifanyika Gabon,
ilikuwa ikifanyika kuanzia katikati ya Januari hadi Februari. Mbali na
kuzitoa Fainali za AFCON katikati ya mwaka hadi mwanzoni, pia idadi ya
timu za kushiriki zimeongezwa kutoka 16 hadi 24 ambako sasa utakuwa na
timu washindwa 10 badala ya mbili kama ilivyokuwa awali.
“Watanzania
wasikate tamaa, hata kama kwa mfumo wa sasa unaofutwa au tuseme
kubadilishwa, bado tuna malengo yetu yalikuwa ni kufuzu, Tunajipanga kwa
hali ya sasa na hatujaanza vibaya na Lesotho. Bado tuna nafasi,”
amesema Karia.
Michuano hiyo kuhamishwa kutoka Januari na Februari hadi Juni na Julai kuanzia Fainali za mwaka 2019 nchini Cameroon.
Hii
si mara ya kwanza kwa Tenga aliyepata kuwa Mwenyekiti wa Baraza la
Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), bali amekuwa
akiteuliwa mara kwa mara kuwa Mjumbe wa Kamati mbalimbali za CAF.
Hongera sana Rais wa Heshima wa TFF, Leodegar Chilla Tenga.
BAHATI HAIKUWA UPANDE WETU - KOCHA
Kocha
Msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania, Fulgence Novatus, amesema kwamba
Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti ya SBL haikuwa na
bahati katika mchezo dhidi ya Amavubi ya Rwanda uliofanyika Uwanja wa
Kigali ulioko kata ya Nyamirambo.
“Tumecheza
vema, tulitafuta nafasi za kutosha. Tumeshambulia sana na kumiliki
mpira. Lakini kila tulipojaribu kufunga, bahati haikuwa kwetu,” amesema
Novatus mara baada ya mchezo huo.
Matokeo
ya sare tasa ya jana yanawapa nafasi ya kusonga mbele Rwanda baada ya
sare ya 1-1 katika mchezo uliofanyika Julai 15, mwaka huu kwenye Uwanja
wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mchezo
huo ni wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa
wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) na sasa Rwanda itacheza na
Uganda mwezi ujao.
Pamoja
na kushindwa kusonge mbele, Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya
Serengeti, imeendeleza rekodi yake ya kutopoteza mechi baada ya kucheza
mechi 11 za kimataifa na kushinda mitano; kutoka sare mitano na kufungwa
mmoja wa nusu fainali za Cosafa.
EmoticonEmoticon