WAZIRI LUKUVI AMSIMAMISHA MUWEKEZAJI WA MKONGE MKOANI TANGA.

July 20, 2017

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wakazi wa kata ya Mnazi wilaya ya Lushoto mkoni Tanga waliozuia msafara wake na kumpa malalamiko kuhusu mashamba matatu yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo bila kuendelezwa na kusababisha migogoro. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikagua mashamba ya katani yanayomilikiwa na kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited yaliyopo kata ya Mnazi wilayani Lushoto mkoani Tanga. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikagua miundombinu na mazingira ya kazi ya mwekezaji wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ambaye ameshindwa kuindeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997. 
Mazingira ya shamba yaliyotelekezwa na mmiliki wake wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ambaye ameshindwa kuindeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na Kamishna wa Ardhi Kanda ya Kaskazini Bwana Leo Komba kuhusu hatua zilizochukuliwa na ofisi yake hadi sasa kwa mmiliki ambae ameshindwa kuwa na sifa za umiliki na hajalipa kodi ya ardhi tangu mwaka 2004 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wakazi wa kata ya Mnazi wilayani Lushoto mkoani Tanga kuhusu shamba hilo linalostahili kufutwa kama ilivyopendekezwa na ofisi ya Mkoa wa Tanga na ofisi ya Kamishna wa Ardhi Kanda ya Kaskazini kwa kuwa mmiliki. 
Baadhi ya mitambo iliyochakaa ambayo mwekezaji wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ameshindwa kuiendeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo hiyo kutoka kwa mkoloni tangu mwaka 1937. 
Baadhi ya mitambo iliyochakaa ambayo mwekezaji wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ameshindwa kuiendeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo hiyo kutoka kwa mkoloni tangu mwaka 1937.
……………………………………………………………………………..
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesimamisha umiliki wa mwekezaji wa mashamba ya katani yanayomilikiwa na kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited yaliyopo kata ya Mnazi wilayani Lushoto mkoani Tanga.
Waziri Lukuvi amefikia uamuzi huo baada ya wakazi wa eneo hilo kuzuia msafara wake na kupata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi hao na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto wakimlalamikia Waziri kuhusu mashamba matatu ya Mnazi yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo bila kuendelezwa na kusababisha migogoro kwa awakazi wa Mnazi.
Baada ya kupokea malalamiko hao Waziri Lukuvi aliamua kutembelea mashamba hayo na kuyakagua ili kujionea hali halisi na kuwasikiliza wananchi ambao wamekuwa wanakabiliwa na mgogoro huu kwa miaka mingi.
Baada ya kutembelea na kujiridhisha Waziri Lukuvi amesema kwamba shamba hilo linastahili kufutwa kama ilivyopendekezwa na ofisi ya Mkoa wa Tanga na ofisi ya Kamishna wa Ardhi Kanda ya Kaskazini kwa kuwa mmiliki ameshindwa kuwa na sifa za umiliki kwa kuwa hajalipa kodi ya ardhi tangu mwaka 2004, hajalipa wafanyakazi wake kwa muda mrefu, miundombinu yake na mazingira ya kazi hayaridhishi na ameshindwa kuliendeleza shamba hilo tangu akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo ileile ya mkoloni ya mwaka 1937.
Aidha, katika ziara hii Waziri Lukuvi amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera ili kutatua migogoro ya mipaka iliopo kati ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara na Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga ikiwa ni muendelezo wa mikutano ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huu ambao umesababisha uvunjifu wa amani.
Waziri Lukuvi anatekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Khassim Majaliwa ambae alimuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kutatua mgogoro huu uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili pindi alipofanya ziara yake mkoani Tanga.
Mnamo tarehe 18 Januari, 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya ziara Wilayani Kilindi katika Kijiji cha Mafisa na kuzungumza na wanachi Kijijini hapo kuhusiana na mgogoro huo na kutoa maagizo kwa viongozi wa kuchaguliwa kuacha kutumia nafasi zao vibaya kuongoza kwa mihemko au ushabiki kwa kuwa kufanya hivyo kunapelekea wananchi kufuata ushabiki na kuvunja sheria zilizopo.
Ili kutekeleza agizo hili wakuu wa mikoa hii miwili wakiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wamekutana ikiwa ni muendelezo wa vikao vya kulitafutia ufumbuzi suala hili.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »