TAARIFA YA KAMATI YA UCHAGUZI TAFCA
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania
(TAFCA), Ramadhani Mambosasa ametangaza majina manane ya wagombea
waliopitishwa katika usaili katika mchakato uchaguzi unaotarajiwa
kufanyika Agosti 10, mwaka huu mjini Dodoma.
Waliopitishwa
kuwania nafasi mbalimbali za uongozi - ngazi ya taifa ni pamoja na
Kidao Wilfred, Lisiter Manyara, Michael Bundala, Dismas Haonga, Jamhuri
Kihwelo, George Komba, Samuel Moja na Mwalwasi.
Nafasi
zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu
Msaidizi, Mweka Hazina, Wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati
ya Utendaji.
WAGANDA KUWACHEZESHA RWANDA, TANZANIA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limewateua waamuzi wa Uganda kuchezesha
mchezo wa marudiano kati ya Amavubi ya Rwanda na Taifa Stars ya
Tanzania. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba,
Mwanza timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Mchezo
huo utakaofanyika Uwanja wa Nyamirambo, Jumamosi saa 10.00 jioni kwa
saa za Rwanda sawa na saa 9.00 alasiri kwa saa za Tanzania, utachezeshwa
na Brian Nsubuga Miiro ambaye atakuwa na jukumu la kupiliza kipenga.
Waamuzi
wasaidizi watakuwa Ronald Katenya (Line 1) na Dick Okello (Line 2)
wakati Mwamuzi wa akiba atakuwa Chelanget Ali Sabila huku Kamishna wa
mchezo atakuwa Ali Mohamed Ahmed kutoka Somalia.
Mchezo
huo ni wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa
wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN). Timu hiyo kwa mwaka huu
imecheza mechi 10 za kimataifa na kushinda mitano; kutoka sare minne na
kufungwa mmoja wa nusu fainali za Cosafa.
EmoticonEmoticon