Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Umoja wa Viijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM ) umesema vijana wanaoendelea kulalamika bila kufanya kazi, kujituma na kutoa jasho la uchapakazi watakawia sana kufikia malengo chanya na kujikwamua hatimaye maisha.
Hayo yameelezwa jana kaimu katibu mkuu shaka Hamdu Shaka alipotembelea kikundi cha ujasiriamali katika kata ya Mwandiga wilaya ya Kigoma vijijini Mkoani hapa .
Shaka alisema hakuna njia mbadala na ya mkato ya kujikwamua kimaisha na hali ngumu yoyote ya umasikini bila kijana mwenyewe kuamua kujishughulisha na kuzalisha mali hatimaye kujitegemea.
Aliwasifu wana kikundi hicho kwa kujikusanya, kupanga mipango na mikakati ya mradi wa kufyatua matofali, kuzalisha sabuni na kuwa na kikundi cha Vicoba kwa mtimdo wa kuweka na kukopa pia kununu hisa.
"Vijana wengi huwa wanawaza, wanapanga na kutaka kutenda hawatendi, kikundi hiki ni makini na kimeamua kuonyesha kwa vitendo jinsi kilivyopania kujikwamua na umasikini wa vipato hatimaye kujijenga kiuchumi "Alisema Shaka .
Shaka aliwahimiza watendaji wa halmashauri ya Kigoma vijijini kuona haja ya kukipa umuhimu kikundi hicho kwa kuwapatia wataalam, mitaji na vyanzo vya fedha.
"Vijana mnakawia, jiungeni ili kushiriki katika shughuli za ujasiriamli kwa lengo la kuacha utegemezi badala yake mjiajiri na kujitegemea kiuchumi kama kikundi cha "Alisema
Kaimu Katibu Mkuu pia alizindua kazi za uchimbaji wa mitaro kwa akili ya usambazaji wa maji safi na salama katika kata ya kalinzi na kutazama maendeleo ya mradi wa ujenzi wa tangi la maji hatimaye akazumgumza na wanachama katika kikao cha ndani katika kata Mgaraganza mkoani hapa .
Kwa upande wake Mbunge wa vijana Mkoa Kigoma Zainab Katimba ameahidi kukisaidia kikundi hicho kwa kuwapatia vyerehani vitano ili kuongeza mradi mwingine wa ushonaji kwa kina dada wa kikundi hicho.
Aliwaeleza vijana hao waendelee na shime hiyo ya kujitolea na kutumia nguvu zao ili kufikia malengo yao ya kujijenga kiuchumi na kupata maisha bora.
"Ingelikuwa vijana wote kigoma na Tanzania wanapitisha maamuzi mazito kama kikundi hiki, nchi yetu isingekuwa na vijana wanaolalamika, wanaosaka ajira au kulalamikia umasikini "Alisema Zainab.
Hata hivyo Mbunge huyo alisema atafanya kila linalowezekana kuhakikisha vijana hao halmshauri ya Kigoma vijijini inawafuatilia na kuwatazama kwa macho mawili makoni vijana hao.
EmoticonEmoticon