Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiwa na mchanga mkononi akiwasikiliza maafisa
wataalam katikati Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye pia ni
katibu wake Bw. Daniel Sagata, na kulia ni Afisa kutoka DAWASA Bw. Abel Chibelenge
akieleza kuhusu uharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi kati kati ya mto Mpigi
katika eneo la Mpaka wa Bagamoyo na Dar es Salaam, ambapo uharibifu huo
Umeharibu eneo ambapo limepita Bomba kubwa la maji safi (halipo pichani) linalo
safirisha maji kutoka Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini na kuhudunia seheu
ya mkoa mkoa wa Pwani na Jiji la Dar es Salaam, Bomba ambalo lipo hatarini
kuharibika.
Afisa Mtaalam kutoka DAWASA Bw. Abel Chibelenje (kulia)
akimuonyesha Naibu Waziri Mpina Sehemu ya mto Mpigi ( haipo Pichani,
iliyoharibiwa vibaya kutokana na shughuli za uchimbaji wa mchanga. (Picha na Evelyn Mkokoi)
NA; EVELYN MKOKOI
Katika hali isiyoya kawaida, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amefanya ziara ya Oparesheni
maalum kwa kushirikiana na jeshi la Police kitengo cha FFU ili kuweza kubaini
uharibifu wa mazingira unaofanywa kwa uchimbani na uchotaji wa mchanga katika
vyanzo vya maji na maeneo mengine.
Akiwa katikati ya Mto Mpigi uliopo katika mpaka wa Dar es
salaam na Bagamoyo usiku wa kuamkia leo, naibu Waziri Mpina alisema kuwa watu
wanaochimba na kuchota mchanga kiholelea watachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni
pamoja na kutozwa faini kwa mujibu wa sheria, kutaifishwa kwa magari yao na
hata kufikishwa mahakamani.
“kama mnavyoona hapa na kama tulivyosikia kutoka kwa mtu wa
DAWASA haya mabomba ya maji yanayopita katika mito yanaharibika kutokana na
shughuli hizi na serikali inaweza kuingia gharama kubwa sana kurekebisha
mabomba haya kama bomba hili Mtaalam amesema hapa itagharimu kiasi cha zaidi ya
shilingi milioni 80 kutengeneza bomba hili.” Alisema Mpina.
Aidha Mpina alisema ukiachilia mbali uharibifu wa Miundo
Mbinu hiyo ya Maji pamoja na Mazingira wananchi wnaweza pia kukosa maji kwa
takribani muda wa wiki mbili.
“Mabomba haya yalikuwa chini ya mchanga lakini kwa sasa hivi
yananing’inia kutokana na uchimbaji wa mchanga na mto unazidi kupanuka na maji
yanakwenda kwenye makazi ya watu na kusababisha mafuriko, na madhara kwa
miundombinu mingine kama vile ya umeme na barabara ambapo serikali imeijenga
kwa gharama kubwa”. Alisisitiza Mpina
Alongeza kwa kusema kuwa hakuna mtu yoyote atakaye ruhusiwa
kuchimba mchanga katika maeneo yasiyo ruhusiwa na wanachi wajihepushe na
uharibifu wa mazingira Mpina alisisitiza kuwa serikali haizuii wananchi
kuchimba mchanga bali inakataza wanachi kuchimba mchanga kiholela na kuharibu
mazingira.
Naibu Waziri Mpina alisema kuwa uungwaji mkono wa sehemu
nyingine ya serikali kama vile Halmashauri na vyombo vingine vya ulizi na
usalama ni mkubwa na ndo maana katika opareshi hiyo hawakuweza kukuta shughuli
zozote zikiendelea katika muda huo,na wahalifu wameanza kuona kuwa serikali
haina mzaha na ndiyo maana team ya oparesheni hiyo imekuwepo katika eneo la
tukio kwa muda huo wa usiku.
“Oparesheni hii ni agizo na zoezi hili litaenda Nchi nzima,
na tumeanzia Dar es Salaam
, Halmashauri zote zinatakiwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya kufanyika kwa
shughuli hii.” Aliongeza Mpina.
Aliwaasa viongozi wasingojee Waziri NEMC au wa Viongozi wajuu
kuwatembelea na kufanya zoezi hili.
Kwa upande wake Afisa kutoka DAWASA Bwana Abel Chibelene wao
kama wamiliki wamiundombinu hiyo ya maji kwa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani
wamefanya jitihada za kutosha kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzai na
usalama, na kufikia hatua ya kuweka walinzia katika miundombinu hiyo lakini
bado wananchi wamekuwa wakiendelea na shugulizi hizo ambazo si salama kwa
mazingira na miundombinu hiyo muhimu ya maji.
Opareshi hiyo ya kamata kamata ya wachimba mchanga,
imeanzishwa na Naibu Waziri Mpina na kuwa ni agizo kwa Halmashauri zote na miji
nchini kutekeleza zoezi hilo
EmoticonEmoticon