Mkuu wa Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Geofrey Ngupula akizungumza na maofisa ugani na waandishi wa habari wilayani humo leo, wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya maofisa ugani yalioandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknojia (OFAB), yenye lengo la kuwakumbusha wataalamu hao wa kilimo nafasi yao pamoja na kuwapatia mbinu mpya za kisasa katika kulima mazao ya Mihogo, Pamba na Viazi lishe katika kuelekea serikali ya viwanda. Kulia ni Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) wa wilaya hiyo, Arafa Njechele na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, Kiwele Michael.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Geofrey Ngupula akizungumza na maofisa ugani na waandishi wa habari ofisini kwake.
Kaimu Mkurugenzi wa wilaya hiyo Hadija Kabojela akizungumza katika mafunzo hayo.
Mtafiti wa Kilimo kutoka COSTEC, Bestina Daniel akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH.
Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Onesmo Kisoka akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mshauri wa masuala ya Bioteknolojia kutoka Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange akitoa mada kuhusu umuhimu wa matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo.
Mratibu wa Jukwaa la Biotehnolojia kwa maendeleo ya kilimo nchini (OFAB), Philbert Nyinondi akitoa ufafanuzi wakati wataalamu hao wa kilimo walipokuwa wakijitambulisha kwa mkuu wa wilaya.
Maofisa Ugani wakiwa katika mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Usikivu katika mafunzo hayo.
Maofisa Ugani ndani ya mafunzo.
Mratibu wa Jukwaa la Biotehnolojia kwa maendeleo ya kilimo nchini (OFAB), Philbert Nyinondi, akiteta jambo na Mtafiti wa kilimo, Bestina Daniel.
Meza Kuu.
Taswira ya ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega wakati wa mafunzo hayo.
Hapa mafunzo yanaendelea. |
Picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mbele alievaa kaunda suti.
Na Dotto Mwaibale, Nzega
TANZANIA ya Viwanda itafanikiwa kwa kuzingatia kilimo cha kitafiti na tafiti za watalaamu na kuachana na kilimo cha mazoea.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Geofrey Ngupula wilayani humo leo asubuhi wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya maofisa ugani wa wilaya hiyo yalioandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknojia (OFAB), yenye lengo la kuwakumbusha wataalamu hao wa kilimo nafasi yao pamoja na kuwapatia mbinu mpya za kisasa katika kulima mazao ya Mihogo, Pamba na Viazi lishe katika kuelekea uchumi wa viwanda nchini.
Alisema kuwa inaaminika kuwa zaidi ya asilimia sabini na tano ya watanzania ni wakulima huku zaidi ya robo tatu wakilima kimazoea na kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kilimo kinaendelea kumdidimiza mkulima na kukifanya kilimo kuajiri
idadi kubwa ya mafukara.
Alisema Teknolojia ya Uhandisijeni (GMO) inafanya vizuri duniani kote hivyo nchi inatakiwa kuitekeleza ili kuyafikia mapinduizi halisi ya kilimo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayo leta ukame, magonjwa na wadudu sugu wahalibifu wa mazao.
Katika hatua nyingine Ngupula aliwataka maofisa ugani kubadilika ili kuendana namabadiliko ya teknolojia ya kilimo katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kilimo.
Akizungumza wakati akitoa mada kwa maofisa ugani hao kuhusu matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo Mshauri wa masuala ya Bioteknolojia kutoka Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange alisema teknolojia hiyo imeleta mapinduzi
ya kilimo kwa nchi ambazo imeanza kuitumia hivyo wakati sasa ufike wa kuanza kuitumia hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa wilaya hiyo Hadija Kabojela aliwaomba watafiti wa kilimo kuzalisha kwa wingi mbegu za mhogo ili ziwafikie wakulima kwa wakati wakati wa msimu wa kilimo hicho.
"Kunachangamoto kubwa ya kupata mbegu bora hivyo ni vizuri mbegu zilizofanyiwa utafiti katika vituo vya utafiti zikawafikia wananchi kwa wakati jambo litakalosaidia wakulima kuacha kutumia mbegu duni zisizo na tija" alisema Kabojela.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Mtafiti wa Kilimo, Bestina Daniel alisema mafunzo hayo ni moja ya utekelezajiwa kazi za COSTECH za kuwawezesha wakulima na wagani katika kutumia mbinu na teknolojia bora za kilimo kwenye uzalishaji ili kuongeza tija na
kupunguza umasikini kwenye kaya.
Alisema Costech ndio wenye dhamani ya kuishauri Serikali kwenye masuala yote yanayohusu Sayansi na Teknolojia hivyo pale kunapotokea teknolojia na mbinu nzuri
ambazo zinaweza kuleta mageuzi kwenye uzalishaji kwa wakulima hutafuta mbinu mbalimbali za kuzifikisha kwa wahusiaka.
Aliongeza kuwa ili kufikia kwenye uchumi wa viwanda lazima malighafi za kutosha ziwepo ili kulisha viwanda hivyo na kuzalisha bidhaa hivyo mazao hayo ambayo
Costech inayahamasisha yatasaidia sana katika kulisha viwanda vya nguo,usindikaji wa mihogo na viazi lishe ambavyo vina umuhimu mkubwa kwenye kuongeza lishe na usalama wa chakula.
Mafunzo hayo ya siku moja kwa maofisa ugani hao yanalenga kuwapatia mbinu bora za uzalishaji wa mazao ya Mihogo,Viazi lishe pamoja na Pamba na nafasi ya matumizi bioteknolojia kwenye kuongeza uzalishaji na kutatua changamoto za kilimo kama magonjwa,wadudu na matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi.
EmoticonEmoticon