Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kushoto) akimvalisha cheo cha Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo
Zanzibar Nd,Ali Abdalla Ali katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa
Ikulu Mjini Unguja kabla alikuwa Naibu Kamishana.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kushoto) akimuapisha Nd,Ali Abdalla Ali kuwa Kamishana Mkuu wa Chuo
cha Mafunzo Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu
Mjini Unguja kabla alikuwa Naibu Kamishana.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kushoto) akimuapisha Kanal Ali Mtumweni Hamad kuwa Mkuu wa Kikosi
cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar (JKU ) katika hafla iliyofanyika
leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza
la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid ni miongoni mwa Viongozi
waliohudhurika katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu
wa Chuo cha Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Baadhi
ya Makamanda wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi JKU na Chuo cha
Mafunzo Zanzibar wakiwa katika hafla ya kuwapishwa wakuu wao Wapya na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein (hayupo pichani) katika Ukumbi wa wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Jaji
Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu (kulia) Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar Mhe.Said Hassan Said na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi
Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud, ni miongoni mwa Viongozi waliohudhurika
katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha
Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara
Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri (kushoto) Mufti Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Saleh Omar Kabi na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, ni
miongoni mwa Viongozi waliohudhurika katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa
JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini
Unguja leo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbali mbali wa
Serikali baada ya kuwaapisha rasmi Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo
Zanzibar Ali Abdalla Ali kuwa (wa nne kushoto) na Kanal Ali Mtumweni
Hamad Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar JKU (wa
nne kulia) hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
(Picha na Ikulu)
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
leo amewaapisha Viongozi wa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
(SMZ), aliowateua hivi karibuni kuwa Wakuu katika Vikosi hivyo.
Katika
hafla hiyo, Dk. Shein kabla ya kumuapisha Naibu Kamishna wa Chuo cha
Mafunzo Ali Abdalla Ali, alimfisha cheo cha Ukamishna na baadae
kumuapisha kuwa Kamishna wa Chuo cha Mafunzo, Zanzibar.
Wakati huo huo, Dk. Shein, amemuapisha Kanal Ali Mtumweni Hamad kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar (JKU).
Hafla
hiyo, ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali
mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Spika wa
Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar
Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said,
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara
Maalum za (SMZ), Haji Omar Kheir, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na
Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.
Wengine
ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Wakuu wa
Vikosi vya SMZ, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman
Khatib, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa
Serikali.
EmoticonEmoticon