Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya.
………………………………………………………………………..
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewataka Wakuu wa wilaya kuacha historia
katika utendaji wao (legacy) kwenye maeneo wanayoongoza.
Naibu Waziri Jafo aliyasema hayo
mjini Morogoro alipokuwa akifungua semina kwa Wakuu wa wilaya ya
kuwajengea uwezo katika usimamizi wa Miradi ya Maendeleo katika sekta ya
Kilimo awamu ya pili(ASDPII) itakayotekelezwa kwa kipindi cha mwaka
2017/2018 hadi 2027/2028.
Akifungua semina hiyo, Jafo
amewataka wakuu hao washindane katika kufanikisha Mipango ya maendeleo
ya serikali ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Kadhalika, amewataka wakurugenzi
wa Halmashauri kuwapa taarifa za fedha za maendeleo ya miradi hiyo
wakati wa utekelezaji ili wakuu hao wa wilaya waweze kufuatilia mwenendo
wa utekelezaji wa Miradi hiyo.
Jafo amesisitiza kwamba katika
kipindi cha hichi ambacho kuelekea uchumi wa viwanda hapa nchini sekta
ya kilimo ndio inategemewa kuzalisha malighafi za viwandani.
Aidha amewataka wakuu hao wa
wilaya kusimamia vyema sekta ya Kilimo ili Tanzania licha ya kutegemea
mazao ya biashara kwa fedha za kigeni sasa Tanzania ijielekeze pia
kuzalisha mazao mengi ya chakula.
Amesema ukifanyika uzalishaji wa mazao ya chakula na ziada ya mazao hayo kuyauza nje ya nchi yataongeza fedha za kigeni nchini.
“Tuna uwezo wa kufanya hivyo kutokana na uwepo wa ardhi ya kutosha yenye rutuba na vyanzo vingi vya Maji,”amesema Jafo
EmoticonEmoticon