BANZI AONYA BIASHARA ZA MAGENDO

May 02, 2017
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Anthony Banzi ameitaka serikali  kuzibiti biashara za magendo kwani madhara yake ni makubwa kiuchumi kutokana na bidhaa za hapa nchini kutopata soko uhakika.

Banzi aliyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na Blog ya Tanga Raha hii ambapo alisema bila kuwepo kwa jitihada za makusudi bidhaa za ndani zitakuwa zikikosa soko hali itakayopelekea kushuka kwa viwango vya uzalishaji badala ya kuongezeka kila wakati.

Alisema suala hilo lina madhara makubwa kiuchumi hivyo mamlaka husika zihakikishe zinalivalia njuga kwa vitendo ikiwemo kuwa mstari wa mbele kupambana nalo ili kuweza kuondosha.

Aidha pia aliwataka watanzania kuunga mkono na jitihada za kupambana na kwa kupiga vita biashara za magendo kutokana na kusababisha bidhaa zetu kukosa soko la uhakika na hivyo kuchangia uzalishaji kushuka.

“Watanzania lazima tuwe wazalendo na bidhaa ambazo zinaza lishwa hapa nchini kwa kuzipa nafasi kubwa ikiwemo kuachana na zile za magendo kwani madhara yake ni makubwa “Alisema Askofu Banzi.

Aidha alisema suala hilo ni moja kati ya mambo ambayo Serikali
inapaswa kulisimamia kwa waledi mkubwa ili liweza kuwa na tija ikiwemo kutoa elimu juu ya athari zake kwa jamii kila wakati.

“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli ipo makini
kuendeleza watu wake kwa kuangalia namna ya kuwajali hivyo nashauri tufundishwe uzalendo kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu”Alisema

Akizungumzia suala la Uvuvi haramu,Askofu Banzi alisema madhara yake ni makubwa hasa kwa vizazi vijazo iwapo hakutakuwa na juhudi za makusudi za kupambana na suala hilo kwa vitendo wakati huu.

“Watu wanatumia uvuvi haramu hii ni hasara kwa Taifa na vizazi vijavyo hasa kiuchumi hivyo jambo hilo lianze kuweka mikakati kabambe ya kulitokomeza kabla halijaleta athari “Alisema.

Aidha pia alishauri kuwepo na utaratibu maalumu kwa wavuvi ambapo kila atakayekwenda kuvua baharini awe na kibali ili kuzibiti uharibifu wa mazingira kuchuma mali kwa kufuja.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »