WAZIRI LUKUVI AZINDUA MPANGO KABAMBE MTWARA

May 02, 2017
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi amefanya uzinduzi wa Mpango Kabambe (Master Plan) ya 2015-2035 Mkoani Mtwara . 
 
Katika shughuli hiyo Mh. Lukuvi aliwataka watendaji wa Mtwara katika sekta ya ardhi kwa kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa Bi. Halima Dendego kuhakikisha kuwa wanafuata Master Plan hiyo ili kuweza kuipanga Mtwara na kanda ya kusini yote vizuri hatimaye kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati na Viwanda.

Katika ziara hiyo, mbali na kuzindua mpango kabambe pia alifanya ukaguzi katika mifumo ya ukusanyaji wa kodi ofisi za ardhi za halmashauri ya manispaa ya Mtwara ili kuhakikisha makusanyo ya kodi ya ardhi yanafanyika kwa malengo mahususi.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego akiongea na wananchi mbele ya Waziri Lukuvi, alimhakikishia Mheshimiwa Waziri kuwa atasimamia utekelezaji wa mpango kabambe kikamilifu kwa maendeleo ya watu wa Mtwara  na watanzania kwa ujumla.

Katika uzinduzi huo Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji na Vijiji, Bi. Imaculate Senje ameeleza kuwa uzinduzi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza au koundoa kabisa tatizo la migogora ya ardhi mkoani mtwara, na kuchochoea fursa za uwekezaji, hivyo amewapa rai wananchi wa Mtwara kufuata mpango huo kwa maendeleo ya taifa.

Pia Ndugu Hamza Sikamkono Afisa Mipango Miji Manispaa ya Mtwara ameeleza kuwa dira ya mpango kabambe huo ni kuwa na mji mahiri wenye uchumi wa mafanikio ambao hutoa kazi na fursa za kutosha na kuvutia uwekezaji.

Afisa huyo ameeleza mpango huo umegusa maeneo ya Naumbu, Mjimwema, Nanguruwe na Ziwani ukigusa huduma zote za kijamii ikiwemo shule na hospitali na shughuli za kiuchumi yakiwemo maeneo ya viwanda na uwekezaji.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Mmanda Baada ya kuwasili mkoani humo.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akizindua mpango kabambe mkoani Mtwara na Mkukabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akikagua mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi katika Halmashauri ya Mtwara ili kuhakikisha makusanyo ya kodi yanafanyika kwa ukamilifu.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akikagua masijala ya ardhi halmashauri ya Manispaa ya Mtwara na kuwataka Maafisa Ardhi kuweka kumbukumbu za Hati Miliki za Ardhi katika mpangilio mzuri ili kuepusha migogoro ya ardhi..
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akiongea na wananchi wa mkoa wa Mtwara katika uzinduzi wa Mpango Kabambe Mkoani hapo.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (wapili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego (wakwanza kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Mmanda (wakwanza kulia), Mwenyekiti wa CCM Mtwara Ndugu Muhamed Sinani (wapili kulia) wakiwa katika uznduzi huo.
 Wananchi wa Mkoa wa Mtwara wakifuatilia Uzinduzi wa Mpango Kabambe (Master Plan) ya Mtwara.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji na Vijiji Bi. Imaculate Senje akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Mtwara.
Ndugu Hamza Sikamkono Afisa Mipango Miji Manispaa ya Mtwara akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Mtwara.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »