Umoja
wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi umesema wakati huu chama na jumuiya
zake kukiwa katika hekaheka za uchaguzi kimewataka wanachama kujitokeza
waaamue kidemorasia kumchagua kiongozi yeyote mwenye sifa na anayefaa.
Pia
umoja huo imeelezea kuwa kila mwanachama ana haki ya kuchukua fomu na
kuwania nafasi ambayo anafikiri ana uwezo nayo katika kuwatumikia
wananchma na chama kwa bidii na maarifa. .
Shaka
alitoa matamshi hayo jana wakati akizumgumza na baadhi ya wajumbe wa
kamati ya siasa uliofanyika kwenye ofisi za ccm wilaya ya Mpanda mkoani
hapa .
Alisema
kazi ya siasa ni ya kujitolea hivyo kila mwanachama anayechukua fomu
kutaka kuwania nafasi yoyote atambue chama kinahitaji mtu mwenye juhudi ,
bidii na utii ili akijenge, kukitumikia na kukitetea kwa nguvu na
hekima.
“Huu
ni wakati muafaka wa kuwapa nafasi wanachama wetu katika ngazi zote
kuamua nankuchagua kwa ridhaa yao, kuwapa viongozi kwa hiari bila
kushawishiwa kwa sababu za kujongwa , rushwa, ahadi au siasa za hadaa
“Alisema Shaka.
Aidha
akizungunza ziara za viongozi wa chama na jumuiya mkoani na wilayani,
alisema ziara hizo ni chama , viongozi wanapita ili kutazama uhai wa
chama na maendeleo yake.
Shaka
alisema anapokuja kiongozi wa chama katika mkoa husika jumuiya zote
zinapaswa kushiriki katika hatua za maandalizi, kupanga na kushiriki
toka mwanzo hadi mwisho .
“Ziara
zote ni za CCM,CCM ina junuiya zake, jumuiya ni watoto wa chama , chama
chetu ni mfano wa mti wenye mizizi mirefu , matawi makubwa yanayotoa
matunda , chama na jumuiya zake wote watoto wa mtu mmoja “Alieleza .
Kaimu
huyo Katibu Mkuu alisems kazi za chama na jumuiya zake ni kuhakikisha
uhai wa chama unaimarika, kuongeza idadi ya wanachama wapya na kufanya
kazi kwa bidii ili kihinde na kuongoza doka.
“Tuendelee
na kazi ya kukipa uhai chama chetu, wsnanchi wanakiamini, wanakiamini
na hawaoni chama mbadala nje ya ccm.,wajibu wetu ni kuwasemea wananchi
katika matatizo ysnayowakabili “Alisistiza Shaka
kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akifungua Shina la wakereketwa la mafundi baiskeli kata ya Majengo wilayan mpanda
Wanachama wa CCM Wilaya ya Mpanda wakishangilia katika Mkutano wa Ndani Wa kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka.
Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa Haidar Sumri akizungumza katika mkutano wa Ndani Wa kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka.
kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akiagana na wananchi mara
baada ya kumaliza Mkutano wa Ndani katika wilaya ya Mpanda Mkoani
katavi.
kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akitoa jezi katika timu
zilizo shinda kombe la MBOGO CUP kwa ufadhili wa Mbunge jimbo la Nsimbo.
kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akikagua Mradi wa kilimo
cha bamia wa Vijana wa kavicha uliopo kata ya kasokola wilayani mpanda
picha na (FAHADI SIRAJI)
EmoticonEmoticon