BALOZI
wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Richard Lupembe, ameweka wazi kuwa
Azam FC ni moja ya timu zinazowatia moyo Watanzania wanoishi nje ya
nchi, huku akiipa mkono wa ushindi kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya
Mbabane Swallows ya Afrika Kusini.
Lupembe
alitoa kauli hiyo wakati alipoitembelea timu hiyo jana kwenye kambi
yake katika Hoteli ya Acardia jijini Pretoria, nchini humo ikijiandaa na
mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa
wa Somhlolo nchini Swaziland Jumapili hii saa 10.30 jioni kwa saa za
Afrika Mashariki.
“Kwa
kweli nimefarijika sana kwa kuiona Azam FC tena kama nakumbuka mlikuja
hapa mwaka jana, mlikuja hapa kucheza na Bidvest nikawa mgeni rasmi na
mkono wangu ukawa wa kheri mkashinda, nawahakikishieni nitawashika tena
mkono na ninauhakika mtashinda tena,” alisema Lupembe
Alisema
kuwa atakuwa pamoja na timu hiyo kwa kipindi chote itakapokuwa jijini
hapa hadi Jumamosi itakapoelekea Swaziland huku akiitakia kila la kheri
kuelekea mtanange huo unaosubiriwa na mashabiki wengi wa timu hizo.
“Ndio
tunafahamu kuwa kuna timu kubwa za Simba na Yanga, lakini Azam FC
inatia moyo kwa sisi watu ambao tulioko nje nawatakia kila la kheri,
mazoezi mema mimi nipo hapa kama balozi, na nitahakikisha nitakuwa na
nyie mpaka siku mtakapoenda kucheza mpira,” alisema,
Lupembe aliitembelea Azam FC jioni wakati ikielekea kwenye mazoezi kujiandaa na mchezo huo.
Mara
mwisho Balozi huyo kuishika mkono Azam FC iliichapa Bidvest Wits mabao
3-0 jijini Johannesburg katika mchezo wa raundi kama hii, ambapo
kutokana na ushindi wa 1-0 katika mchezo wa kwanza kwa sasa timu hiyo
inahitaji ushindi wowote au sare ili iweze kusonga mbele.
Balozi
wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Richard Lupembe akiwa pamoja na
wachezaji wa Azam wakati alipoitembelea timu hiyo jana kwenye kambi yake
katika Hoteli ya Acardia jijini Pretoria, nchini humo ikijiandaa na
mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa
wa Somhlolo nchini Swaziland Jumapili hii saa 10.30 jioni kwa saa za
Afrika Mashariki.alip
Kocha
wa Azam ... akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi ya
kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku ya
Jumapili.
Beki
wa Kulia wa Azam, Shomari Kapombe akiwa anagombania mpira na Kingue
wakati wa mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya
Mbabane Swallows siku ya Jumapili.
Kiungo
wa timu ya Azam, Frank Domayo (kushoto) akijaribu kumtoka mchezaji
mwenzake wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya
Mbabane Swallows siku ya Jumapili.
Nahodha
wa timu ya Azam Himid Mao akijaribu kuutuliza mpira ulipigwa kwake
wakati wa kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku
ya Jumapili.
Ramadhani
Singano akiwa anapambana na Shomari Kapombe wakati wa mazoezi ya
kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku ya
Jumapili.
Makipa wa timu ya Azam wakiwa katika mazoezi.
Wachezaji
wa Azam wakiwa katika mazoezi ya mwisho ya kuelekea mechi yao ya
marudiano dhidi ya Mbabane Swalllows itakayofanyika Jumapili nchini
Swaziland.Picha na Abducado Emmanuel.
EmoticonEmoticon