Taasisi
ya Benjamin W. Mkapa (BMF) jana imekabidhi vitendea kazi (baiskeli 158,
mabegi 150, mabuti 25 na makoti ya mvua 25) vyenye thamani ya Shs
33,985,000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mej. Jenerali (Mstaafu)
Raphaeli Muhuga kwa lengo la kuwasaidia Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na urahisi zaidi.
Taasisi
ya Mkapa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto – Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma pamoja
na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi inatekeleza mradi wa Ukimwi na
Kifua Kikuu chini ya Shirika la Save the Children kupitia ufadhili wa
Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria.
Mradi
huu unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka 3 katika mikoa ya Rukwa, Katavi,
Tabora na Kigoma unalenga kuisaidia Serikali kupunguza maambukizi ya
Kifua kikuu kwa 25% na kupunguza vifo vitokanavyo na Kifua Kikuu kwa 50%
mpaka kufikia 2020. Pamoja na hayo mradi unalenga kupunguza maambukizi
mapya ya Virusi vya Ukimwi, Kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi,
kutokomeza unyanyapaaji na kuongeza upatikanaji wa urahisi wa huduma za
Ukimwi hasa upimaji wa VVU.
Katika
kuhakikisha malengo ya mradi yanafikiwa Taasisi ya Mkapa imetoa mafunzo
mbalimbali katika ngazi ya jamii ikiwemo mafunzo kwa wahudumu wa afya
ngazi ya jamii 183 juu ya ubainishaji na ufuatiliaji wa wagonjwa wa
kifua kikuu ndani ya jamii. Pamoja na hayo jana imekabidhi baiskeli 158,
mabegi 150, mabuti 25, na makoti ya mvua 25 kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi
zitakazotumiwa na wahudumu hao katika utekelezwaji wa majukumu hayo ya
ubainishaji na ufuatiliaji wa wagonjwa wa kifua kikuu na ukimwi kwenye
jamii husika.
Afisa
mradi kutoka Taasisi ya Mkapa Bw. David Magiri akikabidhi nyaraka za
vifaa kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mej. Jenerali (Mstaafu) Raphaeli
Muhuga, kulia kwake ni Katibu Tawala Katavi, Ndg. Paul Chagonja
Bi.
Flora Cosmas, Mhudumu wa Afya ngazi ya Jamii akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Mhe. Mej. Jenerali (Mstaafu) Raphaeli Muhuga, baada ya kupokea
baiskeli iliyotolewa na Taasisi ya Mkapa.
Mkuu
wa Mkoa Katavi Mhe. Mej. Jenerali (Mstaafu) Raphaeli Muhuga, Katibu
Tawala Katavi, Ndg. Paul Chagonja, Afisa Mradi wa Kifua Kikuu na Ukimwi
Taasisi ya Mkapa, Ndg. David Magiri katika picha ya pamoja na Wahudumu
wa Afya ngazi ya Jamii katika halfa ya kukabidhiwa vitendea kazi kutoka
Taasisi ya Mkapa.
Katibu
Tawala Mkoa wa Katavi, Ndg. Paul Chagonja akiendesha moja ya baiskeli
zilizotolewa na Taasisi ya Mkapa kwa lengo la kuwasaidia ufanyaji kazi
wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii mkoa wa Katavi
Hafla ya ukabidhishwaji wa vitendea kazi kwa Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii mkoa wa Katavi.
EmoticonEmoticon