FURAHIA OFA HIZI ZA 'TRAVEL WEDNESDAY' KUTOKA JUMIA TRAVEL

January 13, 2017

Na Jumia Travel Tanzania


Kila siku ya Jumatano ya kila wiki, Jumia Travel (www.travel.jumia.com) huwa inawaletea wateja ofa za punguzo la bei kutoka hoteli mbalimbali nchini Tanzania ambazo hudumu mpaka siku ya Ijumaa.


Ofa hizi humuwezesha mteja kuchagua na kulipia sehemu anayoitaka kwa njia ya mtandaoni au pindi atakapowasili hotelini. Lengo kubwa ni kumuwezesha kila mtu kufurahia utajiri wa sehemu lukuki za kuvutia zinazopatikana kila kona ya nchi kwa gharama nafuu.


Ikiwa ni wiki ya pili tu tangu tuauanze mwaka mpya wa 2017, hoteli zifuatazo zimetoa ofa ya punguzo la bei kuwavutia watu kwenda kufurahia huduma mbalimbali walizonazo.

Mermaids Cove Beach Resort & Spa

Hoteli hii ya kifahari inapatikana Visiwani Zanzibar umbali wa mwendo wa saa moja kutoka mji wa Stone Town ikiwa inapakana na mandhari nzuri ya kuvutia ya bahari ya Hindi. Ukiwa pale unaweza kufurahia huduma kama vile intaneti ya bure, mgahawa uliosheheni vinywaji na vyakula vya kutosha, sehemu ya kufanyia mazoezi, michezo ya kufurahisha, ukumbi wa mikutano na duka dogo la manunuzi.


Nashera Hotel

Hii ni sehemu mojawapo ya zile zinazovutia na unaweza kuanza mwaka huu mpya kwa kwenda kuitembelea. Nashera ni hoteli ya kifahari inapatikana mkoani Morogoro ikiwa inatazamana na mandhari nzuri ya safu ya milima ya Uluguru. Baadhi ya huduma zilizopo ni pamoja na vyakula vya kitanzania na kigeni, simu, vifaa vya kujitengenezea chai au kahawa, sehemu za mapumziko, mashine za kukaushia nywele na ulinzi wa kutosha kwa ajili ya usalama wako na mali zako.  

New Kwetu Hotel 

New Kwetu Hotel inapatikana katika eneo tulivu la Kisosora mkoani Tanga lenye mandhari nzuri na bustani ya kuvutia. Ukiwa hapo utafurahia huduma nzuri za vyakula vya asili na kigeni, mgahawa wenye vinywaji mbalimbali, kufuliwa nguo, usafiri wa kukupeleka uwanja wa ndege na eneo kubwa la kuegeshea magari.

Hoteli zingine zinazotoa ofa hizi ni pamoja na Jangwani Sea Breeze Resort, Golden Tulip Hotel na Skippers Haven za jijini Dar es Salaam pamoja na Paradise Beach Resort na Golden Tulip Zanzibar Boutique Hotel za visiwani Zanzibar.

Kupata taarifa na kufahamu mengi zaidi juu ya hoteli hizi unaweza kutembelea Jumia Travel (www.travel.jumia.com) ili kuweza kuperuzi sehemu utakayoipendelea. 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »