*Awataka viongozi kuwa wawazi
*Awashauri kuanzisha viwanda
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Melinne saccos kuhakikisha
wanakuwa wawazi na kutoa taarifa za hesabu za umoja huo kila wakati ili
wanachama waweze kuwa na takwimu sahihi.
Alitoa
agizo hilo jana jioni (Jumatano, Januari 11, 2017) wakati akizindua
saccos hiyo yenye mtaji wa zaidi ya sh. bilioni moja kwa niaba ya
Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
miaka 53 ya Mapinguzi Matukufu ya Zanzibar.
Waziri
Mkuu alisema viongozi hao wanatakiwa kuwa wawazi kwa wanachama wenzao
jambo ambalo litawajengea uaminifu hivyo kuwezesha umoja huo kudumu na
kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Alisema
vyama vingi vya ushirika nchini vimekufa kutokana na viongozi wake
kutokuwa waaminifu hivyo Serikali hatokubali kuona suala hilo linatokea
katika umoja huo kwani litakwamisha maendeleo.
Aidha,
Waziri Mkuu aliwapongeza wananchi hao kwa kuanzisha saccos hiyo kwani
wameweza kutimiza ndoto ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh
Abeid Amani Karume ya kuondokana na umasikini, dhuluma na unyonge.
Waziri
Mkuu alisema saccos hiyo itawawezesha baadhi ya wanachama kuanzisha
miradi ya ujasiriamali na wengine kuongeza mitaji hivyo kukuza biashara
zao na kuondokana na umasikini.
Awali,
Waziri Mkuu alizindua ukumbi wa kisasa wa mikutano unaomilikiwa na
saccos hiyo na kuwapongeza wananchi hao kwa kubuni miradi ya maendeleo
itayowaongezea kipato na kuweza kujikwamua kiuchumi.
Hata
hivyo aliwataka wanachama hao kuendeleza mshikamano wao na kuendelea
kushirikiana na Serikali ambayo imejipanga kuwawezesha wananchi kiuchumi
kwa kutoa mikopo ya ujasiriamali hasa kwa walio katika vikundi vya
uzalishaji.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu aliwashauri wanachama wa umoja huo kufikiria
uwezekano wa kuanzisha viwanda ili kukuza mitaji yao. Pia vitawezesha
umoja kuongeza za fursa za ajira nchini.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais
wa Zanzibar, Mama Asha Seif Idd kabla ya kufungua ukumbi wa SACCOS ya
Melinne mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shughuli za sherehe ya
Mapinduzi ya Zanzibar
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais
wa Zanzibar, Mama Asha Seif Idd kabla ya kufungua ukumbi wa SACCOS ya
Melinne mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shughuli za sherehe ya
Mapinduzi ya Zanzibar
Waziri
Kassim Majaliwa , viongozi mbalimbali wa serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif
Idd wakati alipozungumza baada ya Waziri Mkuu kufungua SACCOS ya
Melinne mjini Zanzibar
Baadhi
ya wananchama wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua ukumbi wa
SACCOS hiyo
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua SACCOS ya Melinne
mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shamrashamra za sherehe za Mapinduzi ya
Zanzibar januari 11, 2017. Kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Idd
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua SACCOS ya Melinne
mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shamrashamra za sherehe za Mapinduzi ya
Zanzibar
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na
wanachama wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar baada ya kufungua ukumbi wao
Januari 11, 2017. Kulia kwake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,
Balozi Seif Idd.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Idd baada ya kufungua ukumbi wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt. Florens Turuka baada ya kutoka kufungua ukumbi wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt. Florens Turuka baada ya kutoka kufungua ukumbi wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
EmoticonEmoticon