Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Barabara
ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu. Wengine
katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka watatu kutoka kulia Waziri
wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa wakwanza kulia pamoja na viongozi wengine.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi
wengiene akikata utepe kuashiria
uzinduzi rasmi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa mradi wa Barabara ya
Mwigumbi-Maswa (Km 50.3).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo
ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) kutoka kwa Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Cristianus Ako kabla ya kuweka jiwe
la msingi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo
na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuwasili Wilayani
Maswa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mkuu
wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka mara baada ya kuwasili Wilayani Maswa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini
kwenye Ubao kwa kutumia Chaki zinazotengenezwa na Kiwanda cha Chaki cha Maswa
Mkoani Simiyu. Rais Dkt. Magufuli aliwapongeza wenye kiwanda hicho na
kuwashauri kukipanua zaidi ili kiweze kuwafikia Watanzania wengi wenye mahitaji
ya Chaki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiagana na wakazi mbalimbali wa Maswa mara baada ya kumaliza
kuwahutubia Wilayani humo.
Picha namba 14. Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony
Mtaka wakiangalia utengenezwaji wa Chaki katika kiwanda cha Chaki cha Maswa
mkoani Simiyu. PICHA NA IKULU
EmoticonEmoticon