SBL inalaani kusambazwa kwa video isiyo na maadili kwenye mitandao ya kijamii

January 13, 2017



Taarifa kwa vyombo vya habari

Dar es Salaam Januari 12, 2017- Kampuni ya Bia ya Serengeti inapenda kuarifu wateja wake na  umma na kwa ujumla kuwa  video isiyo na maadili   iliyosambaa mtandaoni  ikiwa inaonesha msanii akiigiza  na kuimba wimbo wenye  mahadhi ya taarabu  mbele ya bango la  lenye nembo  Serengeti Premiur Lager haihusiani na wala haikusambazwa na  Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL)..

Tunapenda kuweka bayana kuwa onesho la msanii huyo halikuidhinishwa na SBL Pia  msanii huyo sio sehemu na hajawahi kuwa mmoja wa mawakala wetu wanaotoa huduma za kutangaza bidhaa zetu.

Video hiyo ambayo haikukaa na wala kuzingatia maadili ya sanaa pamoja na maonesho ya wazi inatoa picha mbaya na hata maudhui ya sanaa husika jambo ambalo  haliwezi kufanya na taasisi inayohesimika ndani ya jamii kama SBL.

SBL imekuwa mstari wa mbele  katika kulinda na  kusimamia maadili katika shughuli zake  za kijamii  ikiwa ni pamoja na kuhamasisha  unywaji wa kistaarabu.

Tunauhakikishia umma na wateja wetu kuwa  SBL inafanya shughuli zake za kijamii kwa kuangalia mambo yenye tija kwa jamii na sio vinginevyo.

Tunashukuru sana kwa kuendelea kushirikiana nasi

Imetolewa na

Mkurungezi wa Mkurungezi wa Mahusiano

Serengeti Breweries Limited.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »