Wakati timu pinzani ‘derby’ za JKT Ruvu na Ruvu Shooting
zikitarajiwa kuchuana kesho Ijumaa Januari 13, 2017 kwenye Uwanja wa
Mabatini, ulioko Mlandizi mkoani Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL), Bodi ya Ligi Kuu, imetangaza tarehe rasmi za michezo
mitatu ambayo awali haikupangiwa tarehe katika ratiba.
Mbali ya ‘derby’ ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting, Jumamosi Januari 14,
2017 kutakuwa na mchezo mwingine wa upinzani kati ya Stand United na
Mwadui FC – zote za Shinyanga na zitapambana kwenye Uwanja wa CCM
Kambarage.
Kadhalika siku hiyo ya Jumamosi Januari 14, 2017 Kagera Sugar itakuwa
mwenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
katika mchezo mwingine wa VPL.
Jumapili Januari 15, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja tu wa Ligi Kuu ya
Vodacom ambako Mbao itakuwa mwenyeji wa African Lyon ya Mwanza katika
mchezo utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kadhalika Jumatatu Januari 16, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja tu
ambako Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Toto Africans kwenye Uwanja wa
CCM Kirumba jijini Mwanza.
Michezo mitatu ambayo haikupangiwa tarehe hapo awali kwa alama ya TBA
ikiwa na maana ya kutajwa baadaye (To Be Announced), tayari Bodi ya
Ligi – chombo cha Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF), kinachosimamia na
kuendesha ligi, imepanga tarahe.
Tarehe hizo ni Januari 17, 2017 – siku ya Jumanne kutakuwa na mchezo
mmoja kati ya Majimaji itakayowaalika mabingwa watetezi wa taji la Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Young Africans ya Dar es Salaam katika
mchezo utakaofanyika Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Kadhalika mechi nyingine ziliopangiwa tarehe na muda ni kati ya
Mtibwa Sugar itakayocheza na Simba, Jumatano Januari 18, 2017 kwenye
Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Azam itakuwa mwenyeji wa Mbeya
City kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mchezo huu wa Azam na Mbeya City utaanza saa 1.00 usiku wakati
michezo yote tajwa hapo juu itaanza saa 10.00 jioni lengo likiwa ni
kutoa nafasi kwa mashabiki kushuhudia mechi nyingi kupitia Kituo cha
Televisheni cha Azam - Wadhamini wenza wa ligi hiyo.
Ligi hiyo ambayo pia inabarikiwa na Benki ya Diamond Trust (DTB),
Mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom iliyokuza ubora
wa huduma zake hapa nchini katika mawasiliano ya kupiga simu, kutuma
ujumbe mfupi wa maneno na intaneti yenye kasi.
..…………………………………………………………………………..............
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
EmoticonEmoticon