WANANCHI sasa
wanaweza kulipa malipo ya kodi mbalimbali za Mamlaka ya Mapato nchini
(TRA) kwa kutumia Benki ya NMB. Akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam wakati TRA na NMB walipokuwa wakiingia makubaliano,
Mkuu wa Kitengo cha Miamala wa Benki ya NMB, Michael Mungure alisema
ushirikiano huo umelenga kuwarahisishia raia ulipaji kodi.
Alisema
mwananchi anaweza kulipa kodi mbalimbali za TRA popote alipo kwa
kutumia simu iliyosajiliwa na huduma za kibenki kwa kutumia simu ya
mkononi (NMB Mobile) na kulipa kodi anayoitaji na kama sio mteja pia
anauwezo wa kulipa kodi hiyo kwenye tawi lolote la NMB nchini kote bila
kujali alipo. Alisema makubaliano hayo yanaendelea kurahisisha hali ya
ulipaji kodi kwani.
Benki
ya NMB ina matawi mengi na karibu wilaya zote za Tanzania. Alisema
mtandao wa matawi ya nchi nchini ni mkubwa na imesambaa kwa asilimia 95
katika wilaya zote huku ikiwa na wateja milioni 1.3 wanaotumia mtandao
wa NMB kupitia simu za mkononi 'NMB Mobile' jambo ambalo
litawarahisishia wananchi ulipaji kodi mbalimbali za TRA. Alisema mteja
wa NMB aliyejiunga atatakiwa kupiga *150*66# kisha kuchagua huduma ya
ulipaji kodi kabla ya kufuata maelekezo mengine yatakayomuongoza
kufanikisha malipo ya kodi anayoitaji kulipa.
Imeingia
ubia na TRA kulipa miamala ya kodi popote walipo. Popote alipo usiku au
mchana kulipa kodi zote na ushuru anayoitaka. Sio mpya tumekuwa
tukifanya kipya ni mfumo wa ulipaji sasa kutumia mtandao wetu moja kwa
moja...mfumo wetu utaweza kumuunganisha mteja moja kwa moja na mfumo wa
TRA na kufanya malipo yake. Kwa upande wa TRA, Meneja wa Idara ya
Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi, Ramadhan Sengati alisema kwa
ushirikiano huo na benki ya NMB sasa mifumo ya NMB inazungumza na mifumo
ya TRA moja kwa moja bila usumbufu wowote na kumuwezesha mwananchi
kulipa kodi yake popote alipo.
Aidha
alisema hatua hiyo inaleta unafuu kwa kutosumbuka sana kwa walipaji wa
kodi mbalimbali na kusaidia kuondoa usumbufu. Alisema hatua hiyo pia ni
inaleta usalama wa mtu kutozunguka na fedha mkononi bila sababu jambo
ambalo si salama kwa muhusika. ".
..Hii
itachangia kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi na mfumo bora wa ulipaji,
kwani mteja anaweza kulipa kodi yoyote na hata ushuru na hata wa
kimataifa kwa kutumia mfumo huu popote alipo," alisema Sengati na
kuongeza kuwa; "Malengo yetu ni kurahisisha ulipaji wa kodi ili kujenga
maisha bora, huku ndio tunako enda hivyo tunawashauri wananchi watumie
mfumo huu kulipa kodi mbalimbali za TRA.
EmoticonEmoticon