Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman, akilakiwa na Mhe. Aishieli
Sumari, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi alipowasili
Mahakamani hapo kwa ziara ya kikazi ya kujionea hali ya utendaji kazi
katika Kanda hiyo.
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akisaini kitabu cha wageni
alipowasili katika ofisi ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya
Moshi.
Mhe. Jaji Mkuu akisalimiana na baadhi ya Watumishi wa Mahakama, Kanda alipowasili mapema Julai 14, 2016 kwa ziara ya kikazi.
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akikata utepe kuashiria
uzinduzi rasmi wa Mahakama ya Mwanzo Bomang’ombe iliyopo Wilayani Siha
Manispaa ya Moshi.
Muonekano
wa jengo la Mahakama ya Mwanzo, Bomang’ombe. Mahakama ya Tanzania ipo
katika maboresho mbalimbali yote yakilenga kuboresha huduma ya utoaji
haki, moja ya kipaumbele cha maboresho hayo ni pamoja na kuboresha
mindombinu yake kama majengo ya Mahakama, lengo ni kuwa na majengo ya
Mahakama za Mwanzo katika kila Kata, Mahakama za Wilaya katika kila
wilaya, mikoa na hata Mahakama Kuu.
Mhe.
Jaji Mkuu akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Mahakama ya Mwanzo
Bomang’ombe baada ya kuizindua rasmi Mahakama hiyo ambayo itakuwa
kimbilio la haki kwa wakazi wa eneo hilo.
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman, akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kanda ya Moshi mara baada ya
uzinduzi rasmi ya Mahakama ya Mwanzo Boang’ombe wilayani Hai. (Picha na
Mahakama ya Tanzania).
EmoticonEmoticon