Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh, Luhaga Mpina akipata maelezo kutoka kwa mbunge wa temeke mh,Abdallah Mtolea kuhusu uchafuzi wa mazingira wilaya ya temeke mapema hii leo
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano
na Mazingira Mh,Luhaga Mpina akipata maelezo kutoka kwa uongozi wa kiwanda
cha bia serengeti alipofanya ziara ya kukagua Mazingira katika eneo
hilo la viwanda linalotuhumiwa kuchafua mazingira.
EVELYN MKOKOI
AFISA HABARI OFISI YA MAMAKU WA RAIS
DAR ES SALAAM
14/7/2016
Kampuni ya usafirishaji ya Kanji Lalji iliyopo mtaa wa Serengeti wilayani
Temeke jijini Dar es Salaam imetozwa faini ya shilingi milioni ishirini
na laki tano, na kutakiwa kulipa faini hiyo ndani ya siku saba, kwa
kosa la kutiririsha maji yenye sumu katika mitaro ya maji ya mvua inayoelekea
kwenye makazi ya watu na mazingira na hivyo kuhatarisha maisha na afya
za viumbe hai.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ametoa
kauli hiyo leo kupitia Baraza la Taifa na Hifadhi ya Mazingira NEMC
katika ziara yake ya kukagua viwanda na usafi wa mazingira jijini dar
es salaam.
Ziara hiyo ya Naibu waziri Mpina, iliyopelekea naibu waziri huyo kuinuka
Ofisini na kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika baadhi ya viwanda hivyo,
imetokana na malalamiko ya baadhi ya wanachi katika maeneo husika hususan
wenye viwanda.
Naibu waziri mpina amesema kuwa kutozwa faini ni hatua ya pili kwa
baadhi ya viwanda baada ya kupewa onyo na maelekezo na NEMC na manispaa,
na aliongeza kuwa kwa kutokutii taasisi za serikali baada ya adhabu
hii hatua itakayofuata ni ya kuvifungia viwanda hivyo.
Kwa upande mwingine Mhe. Mpina amekipongeza kiwanda cha Serengeti
breweries kwa kutii kauli ya serikali kwa kulipa faini iliyotozwa awali
ya kiasi cha shilingi milioni kumi na sita kwa kosa la uchafuzi wa mazingira
na kuwashukuru wakazi wanaozunguka kiwanda cha SBL pamoja na Mbunge
wa TEMEME (CUF) Mhe.Abdallah Mtolea kwa kutoa taarifa za uchafuzi wa
mazingira na kukipa kiwanda hicho siku 45 kufanya marekebisho madogo
madogo ya kimazingira kiwandani hapo.
Aidha, Adhabu nyingine ya uharibifu na uchafuzi wa mazingira imetolewa
kwa wamiliki wa eneo la kampuni ya CI group, ambao ni Prime Liberty
Limited ya kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 15 kwa muda wa
siku saba, na kufanya jumla ya faini za uchafuzi wa mazingira zilizotozwa
kwa siku ya leo kuwa shilingi milioni 39 na laki tano.
EmoticonEmoticon