Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson
akimuonesha Rais Dkt. John Pombe Magufuli sehemu ya Madawati
yaliyotengenezwa na fedha zilizopatikana kutokana na kubana matumizi
kutoka Ofisi ya Bunge katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua
Madawati hayo yaliyotengenezwa na Jeshi la Magereza pamoja na Suma JKT.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
amekaa kwenye moja ya Dawati katika hafla hiyo fupi ya ugawaji wa
Madawati hayo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya Msingi Bunge George
Samwel wakati akiangalia mfano wa darasa ya jinsi madawati hayo
yatakavyo katika katika shule mbalimbali nchini.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge wakwanza kulia Mariam Elias
(darasa la tatu na wapili kutoka kushoto George Samwel mwanafunzi wa
darasa la tano wakiwa wanapiga makofi kabla ya tukio la ugawaji wa
madawati hayo yaliyotokana na kubana matumizi kutoka Ofisi ya Bunge.
Mwanafunzi
wa darasa la tano katika shule ya Msingi Bunge George Samwel akimtajia
Mheshimiwa Rais Jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya
kumuuliza huku Waziri Mkuu akitazama kwa furaha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi
Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu ambaye aliyapokea kwa niaba ya
Wabunge wa majimbo mbalimbali nchini.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Kamati ndogo ya Tume ya huduma za Bunge
inayoshughulika utengenezaji wa madawati. Waliosimama mbele ni Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa,
Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu
pamoja na Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya msingi Bunge mara baada
ya tukio la kukabidhi madawati katika Majimbo mbalimbali nchini. Wengine
katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Spika Dkt. Tulia
Ackson pamoja na Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia baadhi ya Maaskari brass bendi ya Jeshi la Magereza mara
baada ya kukabidhi Madawati.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge katika viwanja
vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Mwanafunzi wa Darasa la tatu katika Shule ya Msingi Bunge Mariam
Samwel wakati akiondoka kwenye viwanja hivyo.
Sehemu ya Madawati yaliyokabidhiwa leo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa
aliyehudhuria hafla hiyo ya ugawaji wa Madawati katika Viwanja vya
Karimjee jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
EmoticonEmoticon