NJOMBE YAONGOZA KWA USAFI WA MAZINGIRA ,MOSHI CHALI.

July 13, 2016

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa watu waliofanya vizuri katika usafi wa Mazingira leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akizungumza juu ya Wizara ilivyojipanga katika suala la usafi wa mazingira katika ya kukabidhi tuzo kwa watu waliofanya vizuri katika usafi wa Mazingira leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akikabidhi Ufunguo wa Gari kwa Mwenyekiti wa Halmshauri Njombe, Valentino Hongoli baada ya kuobuka mshindi wa jumla wa usafi wa mazingira katika kampeni ya usafi, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akifurahi na washindi walioshinda pikipiki katika kampeni ya usafi wa mazingira katika usafi wa mazingira katika hafla iliyofanyika leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Halmashauri ya Njombe wakiwa katika picha ya pamoja na gari waliloshinda katika usafi wa mazingira katika hafla iliyofanyika leo.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Njombe imeibuka kuwa mshindi wa Jumla wa usafi wa mazingira na kuifuta historia ya usafi wa mazingira Halmashari ya Moshi kwa kushika.

Halmashauri ya Njombe imepata asilimia 97 ya usafi wa  mazingira na kufuatia Halmashauri ya Iringa Mjini kwa asilimia 81.1 .

Akizungumza leo wakati wa kutoa tuzo kwa halmashauri ,Manispaa, Majiji, Miji  pamoja na Vijiji ,Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa Halmashauri ya Njombe haijaripoti hata mgonjwa wa kipindupindu hata mmoja tangu ugonjwa huo ulipotiwe Agasti mwaka jana.

Amesema kuwa Halmashauri hiyo imeweza kuwa na vyoo bora kwa asilimia 95 katika vijiji yake pamoja na kuwa viaa vya kunawia mikono katika vyoo hivyo.

Halmashauri ya Njombe imepata tuzo ya gari aina ya Land Cruiser Hardtop, Kombe, Cheti,pamoja pikipiki katika vijiji vitatu ambavyo vimefanya vizuri katika suala la usafi wa mazingira.
Jiji la Mbeya limeweza kuibuka mshindi  wa kwanza katika majiji kati ya majjiji manne kutokana na kufanya usafi wa mazingira kwa kuweka mifumo ya uhifadhi takataka.

Tuzo ya jijji la Mbeya  ni kikombe ,pikipiki pamoja na cheti huku Halmshauri ya Mji mdogo wa Tundunduma nao ukiibuka kuwa mshindi wa usafi wa mazingira kwa upande wa miji.

Halmashauri zingine zilizopa tuzo hizo ni Kahama,Mpanda ,Kondoa  huku Mkoa wa Dar es Salaam ikimbulia Wilaya Moja ya Kinondoni ambapo zimetunikiwa tuzo ya vikombe, pikipiki pamoja na vyeti.

Kwa upande wa Hospitali za Rufaa iliyoongoza ni  Mount Meru ikifuatia na Hospitali ya Amani katika nafasi ya pili huku Hospitali ya Morogoro ikishika nafasi  ya tatu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema katika mashindano yajayo walioshinda watakuja kuishangilia Dar es Salaam na hawataondoka na vikombe hivyo na gari.

Amesema kuwa kuna jitihada ambazo zinafanyika za kuhakisha jiji la Dar es Salaam linakuwa safi na hatavumiliwa mtu ambaye anachafua mazingira.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »