Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA), 
limeahirisha mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu ya taifa ya 
wanawake ya Rwanda dhidi ya wageni, Tanzania ‘Twiga Stars’ uliokuwa 
ufanyike Jumapili Julai 17, 2016.
Mchezo huo uliandaliwa na FERWAFA na Rais Paul 
Kagame alipendekeza mchezo huo kuwa sehemu ya burudani kwa wakuu 
mbalimbali wa nchi za Afrika wanaotarajiwa kuwa na mkutano wa viongozi 
hao kuanzia kesho Julai 14, 2016.
Kwa mujibu wa barua ya Rais wa FERWAFA, Nzamwita 
Vincent ya Julai 12, 2016 kwenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania 
(TFF), sababu za kuahirisha mchezo huo ni ratiba ya mkutano huo wa 27 wa
 wakuu nchi.
“Tunasikitika kuwataarifu kuwa ile ratiba ya kuwa 
na mchezo wa kirafiki kati ya Rwanda na Tanzania, imefutwa. Tunaomba 
radhi kwa taarifa hii ya ghafla ambayo iko nje ya uwezo wetu 
inayowafikia huku tukijua kwamba mlikuwa tayari mmeandaa timu kwa ajili 
ya mchezo,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
“Hata hivyo tunaahidi kuendelea kufanya mawasiliano ili kupanga tarehe nyingine ya kufanyika mchezo huo,” ilisisitiza barua.
Taarifa hiyo imekuja wakati tayari Twiga Stars 
ilikuwa imeanza maandalizi ya kutosha kwa mchezo huo ambao ulianza 
kuvutia mamia ya mashabiki wa mpira wa miguu wan chi za Afrika 
Mashariki.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA), 
limeahirisha mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu za wanawake za
 Tanzania ‘Twiga Stars’ na wenyeji Rwanda uliokuwa ufanyike Jumapili 
Julai 17, 2016.
Mchezo huo uliandaliwa na FERWAFA na Rais Paul 
Kagame alipendekeza mchezo huo kuwa sehemu ya burudani kwa wakuu 
mbalimbali wa nchi za Afrika wanaotarajiwa kuwa na mkutano wa viongozi 
hao kuanzia kesho Julai 14, 2016.
Kwa mujibu wa barua ya Rais wa FERWAFA, Nzamwita 
Vincent ya Julai 12, 2016 kwenda kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu 
Tanzania (TFF), sababu za kuahirisha mchezo huo ni kuingiliana kwa 
ratiba ya mkutano huo wa 27 wa wakuu nchi za Afrika.
“Tunasikitika kuwataarifu kuwa ile ratiba ya kuwa 
na mchezo wa kirafiki kati ya Rwanda na Tanzania, imefutwa. Tunaomba 
radhi kwa taarifa hii ya ghafla ambayo iko nje ya uwezo wetu 
inayowafikia huku tukijua kwamba mlikuwa tayari mmeandaa timu kwa ajili 
ya mchezo,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
“Hata hivyo tunaahidi kuendelea kufanya 
mawasiliano ili kupanga tarehe nyingine ya kufanyika mchezo huo,” 
ilisisitiza barua iliyosainiwa na Nzamwita Vincent.
Taarifa hiyo imekuja wakati tayari Twiga Stars 
ilikuwa imeanza maandalizi ya kutosha kwa mchezo huo ulioanza kuvutia 
mamia ya mashabiki wa mpira wa miguu wa ncza Afrika Mashariki na kati.
EmoticonEmoticon