Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akisikiliza maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa serikali za mtaa wa (TPDC)Bw, Idrisa Hashimu kuhusu Uchafuzi wa Mazingira Unaofanywa na viwanda katika mtaa huo.
.Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano
na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiwa katika ukaguzi wa Mazingira katika
kiwanda cha MMI steel kinachotuhumiwa Kuchafua mazingira katika mtaa
wa TPDC
EVELYN MKOKOI,DAR ES SALAAM
Kiwanda cha kutengeneza vyuma cha MMI Steel kilichopo katika eneo la viwanda mikocheni
jijini Dar es Salaam, kimetozwa faini ya shilingi milioni kumi na kutakiwa
kulipa faini hiyo baada ya siku saba kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira
na kanuni zake ya mwaka 2004, kwa kutiririsha maji machafu katika maeneo
ya mtaa wa TPDC kwa warioba jijini dar es salaa. Maji ambayo ni hatari
kwa mazingira na viumbe hai.
Adhabu hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipotembelea eneo la mtaa wa viwanda
mikocheni kufuatia uchafuzi wa mazingira unaotokanao na utitiririshaji
wa majitaka katika maeneo hayo.
Wakati huohuo, Shirika la maji safi na majita taka Jijini Dar es Salaam
na Pwani ( Dawasco) limepewa siku kumi na saba kumaliza tatizo
la utiririshaji wa maji taka katika mtaa wa TPDC mikocheni kwa Warioba
jijini Dar es Salaam.
Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri Mpina Baada ya kufanya usafi
jumamosi ya mwisho wa mwezi wa tatu na kutoa siku saba kwa DAWASCO na
NEMC kusimamia suala zima la usafi wa mazingira na agizo lake kuupuzwa.
Awali, Mhe. Mpina alisema kuwa uchafuzi wa mazingira hauwezi kuendelea
kuvumiliwa na lazima hatua za kisheria zichukuliwe, na kuwaasa watendaji
wa taasisi za serikali kuyapa kipaumbele maagizo yanayotolewa na viongozi
wa ngazi za juu za serikali kinyume na hapo ni kutokutii mamlaka. “tasisi
za serikali lazima zifanye kazi kwa kushirikiana kutokana na kwamba
kumekuwa na kutupiana mpira kati ya NEMC, dawasco na Manispaa ya kinondoni
katika suala zima la utatuzi wa uchafuzi wa mazingira katika mtaa wa
TPDC.” Alisema.
Naibu waziri Mpina aliongeza kuwa ifikapo tarehe 30/7/2016
asikutane tena na tatizo la uchafu na harufu mbaya katika mtaa wa TPDC
kwani hali hiyo ni hatari sana kwa afya ya wakazi wa maeneo hayo na
mazingira.
Kwa upande wake DAWASCO ikiwakilishwa na Injinia Erick Jackson alisema
kuwa Tangu muheshimiwa Naibu Waziri Mpina atoe agizo la uondoshwaji
wa majitaka na uboreshwaji wa miundombinu katika mtaa huo, wamekuwa
wakifanya kazi na bado inaendelea na kazi hiyo pamoja na kukabiliwa
na changamoto mbalimbali za kifedha na ufundi.
Hata hivyo uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya kinondoni umelishitaki
shirika la maji safi na maji taka jijini dar es salaam na Pwani DAWASCO
,kiwanda cha MMI steel na Tembo Tiles kwa uchafusi wa mazingira kwa
kutirirsha maji taka.
EmoticonEmoticon