|
Simba dume akiwa anaunguruma |
|
Simba jike akiwa amepumzika kwenye nyasi |
Na Dickson Mulashani
Suala la utalii wa ndani limeonekana kupata mashiko baada ya
wanafunzi wa chuo kikuu cha Stefano Moshi Memorial University College (SMMUCo) kuhamsika
na kuamua kutembelea hifadhi ya taifa ya Ngoro ngoro ili kujionea vivutio vya
kipekee vinavyopatikana humo.
|
Wanafunzi hao wakiwa katika geti la kuingia hifadhi ya Ngoro ngoro |
Akizungumzia safari hiyo mmoja wa wanafunzi hao Emmanuel
Kalenzi amesema waliguswa kupanga ziara hiyo kuunga mkono wadau mbali mbali
wanaohamasisha utalii wa ndani ili kuweza kuwa mabalozi kwa wengine. “Sisi kama
wasomi ndio tunapaswa kuwa mabalozi kwa jamii inayotuzunguka na ili uwe balozi
mzuri basi uwe umashajionea kwa macho” alisema.
|
Nyati dume mwenye umri mkubwa ambaye tayari ametengwa na kundi lake |
|
Ndege aina ya Cranes nao wanapatikana katika eneo la crater |
|
Nyumbu akiwa amepumzika mara baada ya kula nyasi |
|
Watalii wakiwa katika harakati za kupata picha ya simba |
Katika ziara hiyo ambapo wasomi hao walizuru eneo lenye
umaarufu wa aina yake la “Ngoro ngoro Crater” waliweza kujionea mimea,ndege na
wanyama mbali mbali wakiwemo samba, kifaru, nyumbu,pundamilia , fisi, nyati
swala pamoja na ndege kama tai, cranes pamoja na flamingo.
Wito : ziara hii iwe chachu kwa jamii ya kitanzania kwa
ujumla kuwa na utamaduni wa kuvitembelea vivutio vinavyopatikana maeneo
mbalimbali nchini mwetu ili kuwa sehemu ya kukuza sekta ya utalii na kujivunia
upekee wetu kama nchi iliyobarikiwa.
|
Wanafunzi hao wakiwa katika eneo la view point sehemu ambapo watalii huweza kuona eneo la crater kwa upande wa juu |
PICHA ZAIDI
|
Ngiri na mbweha wakinywa maji katika moja ya mabwawa ya asili katika eneo la crater |
|
Fisi wakiwa wamejilaza kando kando ya maji ili kupunguza joto mwilini wakati wa mchana |
Share this
EmoticonEmoticon