Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akiongozwa na Mkuu wa wilaya
ya Mpwapwa Mohamed Utaly kukagua shamba la mihogo la mkulima wa kijiji
cha Nga’mbi wilayani humo Bahati Mtonyi (kushoto), aliyepata mbegu za
muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya
kukabili maafa ya njaa, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa
muhogo kijijini Nga’mbi wilayani Mpwapwa, Bahati Mtonyi, aliyepata mbegu
za muhogo kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya
kukabili maafa ya njaa (kulia kwake) Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George
Lubeleje, (kushoto) Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly na
Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu , Brig.Jen, Mbazi
Msuya, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akiongozwa na Mbunge wa jimbo
la Mpwapwa, George Lubeleje kukagua mashamba ya muhogo kijijini
Nga’mbi wilayani Mpwapwa baada ya wakulima kupewa mbegu za muhogo kutoka
ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa
ya njaa, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa
Gereza la Mpwapwa, John Tembo, jinsi gereza hilo lilivyo panda mbegu za
muhogo kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili
maafa ya njaa wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa upandaji wa
mbegu hizo wilayani Mpwapwa, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akifurahia mihogo iliyovunwa
katika mashamba ya wakulima kijijini Mazae wilayani Mpwapwa baada ya
wakulima kupewa mbegu za muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya
uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa, mara baada ya
kukagua utekelezaji wa upandaji wa mbegu hizo, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akinawishwa mikono na Mkuu wa Gereza la
Mpwapwa, John Tembo, mara baada ya kuonja chakula cha wafungwa wa gereza
hilo, wakati alipotembelea gereza hilo kukagua shamba la mbegu mbegu
za muhogo walizopata kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili
ya kukabili maafa ya njaa tarehe 19 Juni 2016, (Katikati) Mkurugenzi
idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akishiriki kuonja chakula cha wafungwa
wa Gereza la Mpwapwa wakati alipotembelea gereza hilo kukagua shamba la
mbegu za muhogo walizopata kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa
kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa tarehe 19 Juni 2016, (Kulia kwake),
Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje na (kushoto) Mkurugenzi
idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MUU).
WAZIRI
wa ofisi ya waziri mkuu Sera, Bunge vijana ajira kazi na watu wenye
ulemavu Jenista Mhagama, amemwagiza mkuu wa wilaya ya Mpwapwa
kuhakikisha anatumia nguvu katika kuwalazimisha wananchi kulima ili
kukabiliana na tatizo la njaa ambalo limekuwa likiukabili mkoa wa
Dodoma.
Mhagama
aliyasema hayo jana wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea wakulima wa
zao la mhogo ambao walihamasishwa kulima zao hilo linalostahimili ukame
ili kukabiliana na njaa.
Alisema
kuwa katika kuhakikisha tatizo la njaa linakwisha mkuu wa wilaya huyo
anatakiwa kuweka mikakati mipya ambayo itakuwa na tija katika kuhakisha
njaa inakwisha wilayani hapo.
Aidha
alisema kuwa uongozi wa wilaya hiyo unatakiwa kubuni mikakati mipya
tofauti na ile ya zamani ili kutumia nguvu kazi iliyopo katika kushiriki
kilimo na kusaidia kuondokana na tatizo la njaa.
“Kama
mtaendelea na mikakati yenu ya kila siku tatizo la njaa halitakwisha
mnatakiwa hivi sasa kutumia nguvu lazimisheni wananchi walime mazao
yanayostahimilimi ukame kama mihogo na mtama”alisema Mhagama.
Alisema
kuwa ofisi ya waziri mkuu kupitia kitengo cha maafa ilitoa sh. Milioni
35 kwajili ya kununua mbegu za mihogo na mtama kwajili ya wananchi ya
wilaya hiyo waliokuwa wanakabiliwa na baa la njaa.
Aliongeza
kuwa kwa namna alivyo jionea maendeleo ya baadhi ya wakulima waliolima
mihogo wameweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na baa la njaa kwa
kipindi kirefu.
“Kwa
hali hii basi sisi kama ofisi wa waziri mkuu hatuna haja ya kuendelea
kuleta chakula cha msaada tena huku kwakuwa zao la mihogo ambalo sisi
tulileta mbegu imeweza kuwasaidia wakulima kuondokana na njaa lakini pia
wengine wamejenga nyumba na kuezeka kwa bati”alisema Mhagama.
Aidha
Mhagama alisema kuwa kutokana na wakulima hao kuonyesha mafanikio
uongozi wa wilaya hiyo uongeze bidii katika kuhamasisha kilimo cha zao
hilo.
“Inabidi
muwe na hata sheria ambazo zitawalazimisha wananchi kila mmoja wao
kulima heka mbili za muhogo na mbili zingine za mtama na katika hili
msimbembeleze mtu tumieni nguvu ili kuweza kuondokana na na tatizo la
njaa mkoani hapa”alisema.
Hatahivyo
alimwagiza ofisa kilimo wa wilaya Yustina Munishi , kuhakisha idadi ya
wakulima inaongezeka tofauti na iliyopo hivi sasa.
“Hadi
mwakani tarehe kama ya leo nataka kuja kukaguma mashamba zaidi ya 300 na
kama sitayakuta kwa idadi hiyo utakuwa huna kazi afisa kilimo”alisema.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly alisema kuwa
watakipanga kuhamasisha kilimo cha zao hilo la muhogo ambalo limeonekana
kuwa mkombozi wa njaa.
“Katika
kipindi kijacho cha kilimo kupitia mikakati yetu tutahakikisha kila
kaya inalima heka mbili za mhogo na heka mbili za mtama ili kuondokana
na baa la njaa ambalo limekuwa likiikabili wilaya hiyo kila
mwaka”alisema Utaly.
Naye
mmoja wakulima hao Bahati Mtonyi,alisema kuwa kupitia zao hilo la muhogo
ameweza kujenga nyumba na kujilipia ada kila mwaka kiasi cha sh.
600.000.
EmoticonEmoticon