Wakulima wa zao la
Shahiri kanda ya Kaskazini mwa Tanzania wanaoshirikiana na kampuni ya
TBL Group wameadhimisha siku yao wilayani Karatu ambapo mgeni rasmi
katika maadhimisho hayo alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na
Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha wakiwemo wadau wao kutoka
SABMiller,na makampuni mengine yanayouza madawa na pembejeo za kilimo.
Wakulima waliweza kufanya
maonyesho mbalimbali ya kazi zao pia walielezea mafanikio walioweza
kuyapata kutokana na kilimo cha zao la Shahiri
Maofisa
wa SABMiller na wafanyakazi wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja wakati
wa maadhimisho hayo ambapo pia TBL Group ilitunukiwa tuzo kwa kendeleza
kilimo cha zao la Shahiri nchini
Mkuu
wa Uendelezaji Kilimo cha Shahiri wa SABMiller kanda ya Afrika Thinus
Van Schoor akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima wa
Shahiri
Wakulima wa Shahiri wakitembeza wageni mashambani
Naibu
Waziri wa Kilimo,Chakula na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha
(kulia) akimpongeza mkulima aliyejishindia zawadi ya kabati 2/4-Wakulima
wa Shahiri wakitembeza wageni mashambani
Naibu
Waziri wa Kilimo,Chakula na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha
(kushoto) akimpongeza mkulima wa Shayiri kutoka Kijiji cha Lendikinya
wilaya ya Monduli,Masiaya Oloshuda aliyeshinda kwenye bahati nasibu ya
kupata vifaa vya usalama shambani
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha akihutubia wananchi
EmoticonEmoticon