WHO NA JUMUIA YA ALYAMIN WATOA VIFAA VYA KUCHUNGUZIA MAJI NA MAJI YA KUNYWA KATIKA JUHUDI ZA KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU ZANZIBAR.

May 13, 2016

 MWAKILISHI wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Andemichael Ghirmay, akizungumza na Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo alipofika ofisini kwake  kukabidhi Vifaa vya kuchunguzia Maji.
 MWAKISHI wa WHO Zanzibar Dkt. Andemichael Ghirmay akimkabidhi Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo moja ya Vifaa vya kuchunguzia Maji katika  hafla ilioyofanyika Wizara ya Afya Mnazi mmoja mjini Zanzibar.
 MTAALAMU wa Maji wa  WHO Michael Habtu, akikifanyia majaribio kifaa cha kuchunguzia maji huku Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akiangalia kwa furaha.
 MTAALAMU wa Maji kutoka WHO Michael Habtu, akiwaonesha matokeo ya Maji alioyapima kwa kifaa cha kuchunguzia maji huku Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akiangalia, wakwanza (kulia ) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili na Mwakilishi wa WHO Dkt. Andemichael Ghirmay
 SHEHENA ya Msaada wa Maji ya kunywa uliotolewa na Jumuia ya Alyamin kwa ajili ya wagonjwa wa kipindupindu Zanzibar.
MWENYEKITI wa Jumuia ya Alyamin Dkt. Omar Swaleh akimkabidhi Waziri  wa  Afya Mahmoud Thabit Kombo Msaada wa Maji  na vidonge vya kutibu maji ya kunywa kwa ajili ya wagonjwa wa kipindupindu, (kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Juma Malik Akili. 
 
PICHA NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »