Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde leo
amefanya ziara ya kushtukiza katika kambi tiba ya GSM Foundation
inayofanywa na kikosi cha Madaktari bingwa kutoka hospitali ya MOI,
ambayo kuanzia leo imepiga kambi Dodoma baada ya kutoka katika mikoa ya
Mwanza, Singida, na Shinyanga.
Akieleza
sababu za kuitembelea kambi hiyo ambayo iko katika hatua zake za mwisho
kumaliza awamu ya kwanza, Mheshimiwa Mavunde amebainisha kwamba kwanza,
ni kwa sababu alisikia kambi iko katika jimbo lake, lakini jingine
kubwa na la msingi likawa ni kupeleka shukrani zake kwa Maafisa wa
Taasisi ya GSM wanaoambatana na madaktari kuweka kambi tiba hizo katika
kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na migongo wazi
kila mwaka.
“Nimeshtushwa
na takwimu za mwaka juzi, kwamba wanaozaliwa ni 4000 na wanaorudi
hospitali kwa ajili ya tiba hawazidi 600. Hii ni hatari, ilipaswa mtu
kuchukua jukumu la haraka na nimeshukuru kusikia GSM mmefanya hilo,
hongereni sana”, alisema Mavunde.
Mavunde
amewataja Maafisa wa GSM na Madaktari kuwa ni watu wenye moyo wa
kizalendo ambao wanatakiwa kuigwa na jamii, wameacha familia zao, na
wameamua kuokoa maisha ya watoto ambao hata hawawajui, kwa sababu moja
tu kubwa na ya msingi ya utanzania.
PICHANI JUU: Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony
Mavunde(Wa Pili kutoka kulia) akikaribishwa eneo la Hospitali na Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw Jordan Rugimana(Wa tatu kutoka kulia) na
Naibu Mkurugenzi wa MOI ambaye ndio mratibu wa kambi tiba ya GSM DK
Othman KIloloma(Wa nne kutoka kulia) na Meneja wa Taasisi ya GSM BI
Shannon Kiwamba(kushoto)
Mh Mavunde akisikiliza maelezo ya mmoja kati ya wagonjwa waliohudhuria kambi tiba ya GSM
Mratibu wa Kambi Tiba ya GSM, Dk Othman Kiloloma akimpa taarifa za wagonjwa Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini
Mh Mavunde akiongea na wanahabari waliokuwa hospitalini hapo kufuatilia habari za wagonjwa waliohudhuria kambi tiba ya GSM
Mh
Mavunde akibadilishana mawazo na mratibu wa kambi tiba ya GSM, Dk
Othman Kiloloma, wanaosikiliza ni Kibwana Matukio kutoka GSM, na Mganga
mkuu wa mkoa Bw Jordan Rugimana
EmoticonEmoticon