EU YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA

May 11, 2016
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer
Kutoka kushoto ni Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer, Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya (EU) Tanzania, Luana Reale wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa idara mbalimbali katika Ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 66 ya EU duniani (Picha na Modewjiblog)
Umoja wa Ulaya (EU) umesema kuwa utaendelea kushirikiana na Tanzania katika shughuli za maendeleo ikiwa kama ni moja ya kazi wanazozifanya kusaidia ukuaji wa maendeleo katika maeneo mbalimbali duniani.
Hayo yamesemwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer, kwenye halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa kiuchumi, ustawi, Amani na Demokrasia duniani, kuwa kwa kipindi kirefu EU imekuwa ikifanya kazi nchini na hivyo wataendelea kukuza ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya lakini pia kuisaidia Tanzania kuata maendeleo zaidi.
“Tutaendelea kusaidia Tanzania kukuza uchumi, kusaidia kuwepo na usalama na amani na hizo ni kazi ambazo tumekuwa tukizifanya hivyo tunaamini ushirikiano wa Tanzania na EU utaendelea kuwepo kwa kipindi kirefu,” alisema Van de Geer.
Pia alisema wanatambua kazi aliyoifanya Mwalimu Nyerere wakati akiwa madarakani na hata kasi iliyopo sasa katika kuleta maendeleo katika serikali ya Rais Magufuli hivyo wanaamini maendeleo yatapatikana kwa kasi.
Alisema kwa upande wa EU wataendelea kusaidia maendeleo ambapo kwa sasa watahakikisha mradi wa maendeleo wa miaka mitano (2016-2020) utafanikiwa ili kuifanya Tanzania kufikia malengo ya kuwa moja ya nchi iliyo na maendeleo barani Afrika.
Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa chini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer akiamkaribisha Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa chini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla kwenye halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa kiuchumi, ustawi, Amani na Demokrasia duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Roeland Van de Geer EU Tanzania
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer akikaribisha wageni waalikwa kwenye halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa kiuchumi, ustawi, Amani na Demokrasia duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Hoyce Temu UN Tanzania
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer baada ya kuwasili kwenye hafla hiyo.
Felista Rugambwa
Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya (EU) Tanzania, Luana Reale akisalimiana na Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa anayeshughulikia dawati la Marekani na Ulaya Marekani, Felista Rugambwa huku Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer akiendelea kukaribisha wageni waalikwa.
Susanne Mbise
Afisa Habari wa Umoja wa Ulaya, Susanne Mbise akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Balozi wa Umoja huo, Bw. Roeland Van De Geer kuzungumza na wageni waalikwa katika hafla mchapalo ya siku ya Umoja wa Ulaya iliyofanyika tarehe 9 Mei katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Roeland Van de Geer
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani kwenye sherehe ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa Kiuchumi, Ustawi, Amani na Demokrasia duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jiijini Dar es Salaam.
Awa Dabo
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia) akibadilishana mawazo na Balozi wa Uswiss Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arthur Mattli katika hafla hiyo.
Balozi wa Ireland nchini Flonnuala Gilsenan
Balozi wa Ireland nchini, Fionnuala Gilsenan akibadilishana mawazo na Balozi Liberata Mulamula (kushoto) halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa kiuchumi, ustawi, Amani na Demokrasia duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Einar Hebogard Jensen
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Einar Hebogard Jensen (kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.
IMG_4676
Picha juu na chini ni wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali wakiendelea kubadilishana mawazo katika hafla hiyo.
IMG_4772
Stella Rwechungura
Stella Rwechungura wa Umoja wa Ulaya (EU) Tanzania (wa pili kushoto), Clara Swai wa Ubalozi wa Uingereza (wa pili kulia) pamoja na Ameeta Mehta wa EU Tanzania (kulia) katika picha ya pamoja na mmoja wa wageni waalikwa wakati wa halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 tangu kuanzishwa kwake.
Hoyce Temu
Kutoka kushoto ni Afisa mshiriki anayeshuhghulikia Mawasiliano na Ushirikiano wa UN Tanzania, Didi Nafisa, Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu pamoja na Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa anayeshughulikia dawati la Marekani na Ulaya Marekani, Felista Rugambwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 tangu kuzaliwa kwake.
IMG_4761
Pichani juu na chini ni baadhi ya mabalozi na wadau kutoka taasisi za serikali na zisizo za serikali, Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika mbalimbali waliohudhuria hafla ya siku ya Umoja wa Ulaya nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
IMG_4755
IMG_4758
Liberata Mulamula
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kulia) akisalimiana na Balozi Liberata Mulamula wakati halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya (EU) katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa kiuchumi, ustawi, Amani na Demokrasia duniani tangu kuzaliwa kwa umoja huo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »