Taasisi za Umma zatakiwa kutumia mifumo ya kiutendaji

May 11, 2016


SONY DSC
SONY DSC
Wawakilishi kutoka Taasisi mbalimbali za Umma nchini wakifuatilia mada
SONY DSCMkurugenzi Msaidizi Bi. Veila Shoo akiwasilisha matokeo kuhusu Ufuatiliaji wa Mifumo na Viwango vya utendaji kazi kwa Taasisi za Umma nchini.Wanaomsikiliza ni sehemu ya wawakilishi kutoka katika Taasisi za Umma.
……………………………………………………………………………………………….
Taasisi za Umma zimehimizwa kutumia ipasavyo mifumo ya utendaji kazi iliyowekwa ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi Msaidizi ,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Veila Shoo alisema hayo wakati akitoa takwimu za matumizi ya mifumo hiyo katika kikao kazi kilichohusisha wawakilishi kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala za Serikali na kufanyika katika  ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
Bi. Veila alieleza kuwa ufuatiliaji wa mifumo umefanyika katika Idara Zinazojitegemea 16 ambapo imebainika baadhi ya mifumo inatukima ipasavyo wakati mingine bado.
Awali, akifungua kikao kazi hicho Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Bw. Mick Kiliba alisema kuwa zoezi la kufanya ufuatiliaji wa mifumo ni endelevu na watendaji wanatakiwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kutumia mifumo hiyo.
Alisema lengo la tathmini hiyo ni kupata takwimu za utekelezaji wa mifumo na viwango vya utendaji kazi, kutambua mifumo yenye changamoto za utekelezaji, kutoa hamasa ili kuboresha utoaji huduma na kutoa mrejesho kwa taasisi jinsi ya kuimarisha mifumo.
Mifumo iliyofanyiwa tathmini ni pamoja na:- Mpango mkakati Mkataba wa Huduma kwa Mteja; Mfumo wa wazi wa Tathmini ya Utendaji kazi; Uboreshaji wa michakato ya Utoaji huduma; Tathmini ya Utoaji huduma wa Taasisi; Tathmini ya ndani ya Taasisi; Ushirikiano wa Taasisi ya Umma na Asasi za Kiraia(AZAKI); Waraka Namba 1 wa mwaka 2012 kuhusu Ununuzi wa Samani za Ofisi; na   Usimamizi wa Fomu za Serikali.      

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »