NYASA BOY ASHINDWA KUTOA VIDEO YA CHONGOROA KISA HAJAMZOEA VIDEO QUEEN WAKE.

May 01, 2016
Msanii Chipukizi kutoka Jijini Mwanza, "Nyasa Boy" (Kushoto) amesema ilimchukua miezi minne hadi kuzoeana na Mlimbwende "Mwanne" (kulia) ambae ameshiriki kwenye video ya wimbo wake uitwayo "Chongoroa".

"Hii video ingekamilika mwezi wa nne mwaka huu lakini imechelewa baada ya kuahirisha kuishoot mara kwa mara kutokana na kunichukua muda mrefu kuzoeana na video queen wangu". Alisema Nyasa ambae kiuhalisia ana aibu sana alipokuwa akizungumza na BMG.

Video hiyo ambayo imerekodiwa na "Blue Ray Video" chini ya Director "Musta" ilitarajia kutoka mwezi April mwaka huu jambo ambalo limeshindikana kutokana na sababu zilizoelezwa na Nyasa Boy, hivyo inatarajia kutoka mwezi huu wa tano.
Nyasa Boy (kushoto) akiwa Location na Video Queen Mwanne (Kulia).
Bonyeza HAPA Kutazama picha za Chongoroa

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »