Wananchi wa tarafa ya Mwandoya, wilayani Meatu Mkoani Simiyu
wakifanya usafi wa mazingira kwa kufyeka katika eneo la kituo cha afya cha
Wandoya leo, ikiwa ni utekelezaji wa
agizo la serikali la kufanya usafi wa mazingira na kutena jumamosi maalum ya mwisho
wa mwezi kuwa ya usafi wa mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira
mhe. Luhaga Mpina akimwagilia mti baada ya kuupanda Wilayani Meatu Mkoani
Simiyu Leo mara baada ya kuupanda.
EVELYN MKOKOI,SIMIYU 30/4/2016
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano za Mazingira
Mhe. Luhaga Mpina ameshiriki usafi wa mazingira wa kila jumamosi ya mwisho wa
mwezi, mara hii mkoani Simiyu katika wilaya ya Meatu jimboni Kisesa.
Akizungumza na wananchi wa eneo la Mwandoya wilayani Meatu,
Mhe. Mpina amewaasa wananchi wa mkoa wa Simiyu kwa ujumla kuitunza miti
4820 iliyopokelewa na kupandwa wilayani hapo baada ya serikali ya awamu ya
tano kutekeleza ahadi yake ya kuupatia Mkoa wa Simiyu idadi hiyo ya miti.
Naibu Waziri Mpina, alisema kuwa kwa kuwamkoa wa simiyu huko
kwenye hatari kubwa ya kuwa janga na umesha wahi kukabiliwa na tatizo la uhaba
wa chakula, kabla ya uchaguzi uliopita, kwa kuitunza miti hiyo ya matunda wakazi
wa mkoa huo watanufaika na miti ya matunda
hayo ya muda mfupi kwa kufanya biashara ili kuweza kukuza uchumi na
kuongeza kipato cha kila mmoja.
Aliongeza kuwa, zoezi
la upandaji miti mkoani simiyu katika ma shule, maeneo ya makazi ya watu na
mashamba yanahitaji utunzani mkubwa kwani miti hiyo ina uwezo mkubwa wa
kuboresha uoto wa asili ambao mpaka hivi sasa umetoweka.
Aidha Mhe. Mpina amewataka viongozi wa mkoa wa Simiyu
kuchukua nafasi yao kusimamia wanachi wafanye usafi ikiwa ni agizo la serikali
la kila mwisho wa mwezi kuwa siku ya usafi na kuwa viongozi ambao watakuwa
wazembe katika suala zima la usimamiaji wa usafi wa mazingira watachukuliwa
hatua.
Alipoongea na wanachi wa Jimbo La Kisesa, Naibu Waziri Mpina
aliwaasa wananchi wa Kisesa wa sapoti jitihada za serikali za kupanda miti na
kutunza mazingira, na kuwa hakikishia wapiga kura wake kuwa pamoja na kuwa
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, nafasi za kazi yake
kama Mbunge wa jimbo hilo ipo pale pale na ataendelea kuwapigania wana Kisesa.
Aliwaomba wana Kisesa wawe mfano wa kupanda miti iliyotolewa
na serikali na kuitunza na kwa aliokosa miche ya miti hiyo iliyogawiwa ame
ahidi kuwapatia miche mingine kwani shabaya yake kubwa ni kuwezesha mkoa wa simiyu
kupata miti hasa ya matunza na mbao ili kuboresha uchumi binafsi na pato la
taifa.
Mhe. Mpina Amefanya usafi wa mazingira leo katika eneo la
hospital ya Mwandoya pamoja na kupanda miti ikiwa ni sehemu ya utekekezaji wa
kampeni ya kitaifa ya kupanda miti.
EmoticonEmoticon