Baadhi
ya wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, wakishiriki matembezi ya
kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani (May day), hapa matembezi yakiwa barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 1,
2016.
NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MFUKO
wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) kwa mara ya kwanza umeshiriki kwenye matembezi
ya kusherehekea siku ya Wafanyakazi, maarufu kama MAY DAY jijini Dar es Salaam
leo Mei 1, 2016.
Matembezi
hayo yaliyoshirikisha wafanyakazi kutoka sekta ya Umma na Binafsi, ambazo ndio
wadau wakubwa wa Mfuko huo, yalianzia kwenye ofisi za Shirikisho la Vyamavya Wafanyakazi,
TUCTA, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kupita barabara ya Nkurumah, Nyerere
na kisha kupinda barabara ya Chang’ombe hadi uwanja wa Uhuru ambako
yalipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda.
WCF
ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa
kifungu cha 5 cha sheria ya Bunge ya Fidia kwa wafanyakazi namba 20 ya mwaka
2008 ukiwa na wajibu wa kutoa Mafao ya Fidia kwa mfanyakazi apatwapo na madhara
mahala pa kazi.
Tangu
kuanzishwa kwa Mfuko huo, juhudi za kutangaza hudumazake kwa wadau zimekuwa
zikiendelea mfululizokwa kutoa elimu kupitia semina, maonyeshona makongamano
lakini pia kupitia vyombo vyahabari na kwa siku ya Mei Day imekuwa ni fursa
kubwa ya WCF kuungana na wadau wake wakubwa.
Wafanyakazi
wa WCF wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuruwakati wa matembezi ya
kilele chasiku ya wafanyakazi Duniani
Matembezi yakipita barabara ya Chang'ombe
Matembezi yanaendelea, hapa ni barabara ya Uwanja wa Taifa mkabala na ofisi za TAKUKURU wilaya ya Temeke
Matembezi yakiendelea barabara ya Chang'ombe
Matembezi yakiwa barabara ya Uwanaja wa Taifa
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa kwenye matembezi hayo, hapa nibarabara ya Chang'ombe
Baadhi
ya wafanyakazi wa WCF, wakimsikiliza mwenzao aliyevaat-shirtyenye ujumbe maalum
wa Mfuko huo “WCF inatoa Fidia Stahiki kwa Wafanyakazi wote wa Sekta ya Ummana
Binafsi”.
Mkuu wa Mkoa wa Dar esSalaam, Mh. Paul Makonda, (kulia), akiteta jambo na kiongozi wa Shirikisho la Wafanyakazi mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa kilele cha May Day uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa WCF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha
matembezi hayo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa WCF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha
matembezi hayo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Nyuso za furaha baada ya matembezi
EmoticonEmoticon