Timu ya Acacia Stand United fc (CHAMA LA WANA) inayodhaminiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya Dhahabu ya ACACIA,mara baada ya kupoteza mchezo wake wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kufungwa goli 2-1 na Simba Sc,kesho jumatatu inataraji kuingia kambini katika Mgodi wa Dhahabu BUZWAGI kujiandaa na mchezo wake unaofuata dhidi ya Maafande wa jeshi la kujenga taifa JKT Ruvu.
Afisa habari wa klabu hiyo ISAAC
EDWARD amesema kupoteza mchezo wao dhidi ya Simba Sc ni sehemu ya
matokeo ya Mpira wa miguu, kwani hivi sasa ligi ni ngumu na kila timu
inapambana ili kupata matokeo mazuri.
“tumepoteza mchezo wetu tukiwa
nyumbani dhidi ya Simba ni sehemu ya mchezo,tunajipanga na mchezo
unaofata nyumbani ambao tutacheza na Jkt Ruvu , timu inataraji kuingia
kambini siku ya kesho jumatatu katika Hosteli za Mgodi wa Dhahabu
BUZWAGI kujiandaa na mchezo wetu unaofata”
Ameongeza kuwa mchezo ujao timu
hiyo ya Acacia Stand United imejipanga kuhakikisha inapata ushindi ili
wazidi kujiweka sehemu nzuri kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.
“Uongozi pamoja na Benchi la
Ufundi tumejipanga vilivyo ili tupate pointi tatu ambazo zitazidi
kutuweka katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi ”
Isaac amewaomba mashabiki na
wapenzi wa klabu hiyo kuunganisha nguvu kwa pamoja na kuisaidia timu
kupata matokeo mazuri nyumbani na Ugenini.
“ mashabiki wetu na wapenzi wa
Acacia Stand United (Chama la wana) waendelee kuipa timu ushirikiano
katika michezo yetu yote iliyobaki katika mzunguko wa pili ambao ni wa
lala salama ikiwa tunacheza nyumbani na hata ugenini pia ”.
Acacia Stand United Fc kwasasa
imejikusanyia pointi 29 katika michezo yake 18 walioshuka dimbani
katika msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.