Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) halitatangaza timu
iliyopanda Ligi Kuu msimu ujao kutoka Kundi C, mpaka itakapoamuliwa na
vyombo husika vya TFF baada ya michezo ya kundi hilo kuchezwa leo jioni
katika viwanja tofauti nchini.
TFF imefikia hatua hiyo ili kupata nafasi ya kupitia taarifa za
michezo kati ya JKT Kanembwa v Geita Gold na Polisi Tabora v JKT Oljoro
iliyochezwa leo jioni katika mikoa ya Kigoma na Tabora.
Taarifa za michezo hiyo kutoka kwa wasimamizi husika na vyanzo vingine vinakusanywa ili zifanyiwe kazi na vyombo husika vya TFF.
Katika michezo hiyo ya leo, Geita iliibuka na ushindi wa mbao 8 – 0
dhidi ya JKT Kanembwa, huku Polisi Tabora wakiibuka na ushindi wa mabao 7
– 0 dhidi ya JKT Oljoro.