Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba
akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka
wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba
akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka
wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akitoa ufafanuzi kuhusu wizara hiyo leo Bungeni mjini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Hamis Andrea Kigwangalla (kushoto) akiwa Bungeni
leo mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Dkt.
Ashatu Kijaji.
Baadhi
ya Wabunge wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais, Mazingira na Muungano January Makamba (hayupo pichani) alipokuwa
akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa
fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Mwanafunzi
wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini
Mwanza Getrude Clement akiwa Bungeni leo mjini Dodoma kwa mwaliko wa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January
Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango wake kwenye
utunzaji wa mazingira. Mwanafunzi huyo alihutubia viongozi mbalimbali wa
dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia
nchi, uliofanyika New York Marekani.
Mashududa
walihusika katika zoezi la kuchanganya udongo wakati wa Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964, wakiwa Bungeni leo mjini Dodoma
kwa mwaliko wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na
Muungano January Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango
wao katika kuuenzi na kuulinda Muungano wa Tanzania.
Mwanafunzi
wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini
Mwanza Getrude Clement (wa pili kushoto) ambaye alihutubia viongozi
mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu
mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani akiwa na
wanafunzi wenzake Bungeni leo mjini Dodoma.
Naibu
Spika Dkt Tulia Ackson na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,
Mazingira na Muungano Mhe January Makamba wakiwa katika picha ya pamoja
na mashuhuda waliohusika katika zoezi la kuchanganya udogo wakati wa
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964. Mashuhuda hao
walikuja kutembelea Bunge leo Mei 2, 2016.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma)
………………………………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma.
Serikali inaendelea kusimamia
mazingira na kuhakikisha mifuko ya plastiki inayotumika nchini iwe ni
ile inayokidhi viwango vianvyokubalika ili kuondokana na changamoto ya
kuzagaa kwa mifuko hiyo katika maeneo mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni
mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na
Muungano January Makamba alipokuwa akitoa hoja ya wizara yake
kuidhinishiwa maombi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Makamba amesema kuwa sababu kubwa
ya kusambaa kwa mifuko plastiki inatokana na mifuko hiyo kutolewa bure
na hivyo kuchafua mandhari na kuziba mifereji sehemu mbalimbali hali
inayosababisha athari kubwa katika mazingira.
“Asilimia kubwa kwenye mito,
maziwa na fukwe za bahari imejaa mifuko ya plastiki, hali hii ni hari
kwa usalama wa mazingira yetu” alisema Makamba.
Akiwasilisha hotuba yake, Waziri
Makamba amesisitiza kuwa mifuko ya plastiki isiyotakiwa kutumika nchini
ni ile yenye unene chini ya maikroni 50 ambayo hairuhusiwi kuzalishwa
wala kuingizwa.
Kwa mujibu wa maelekezo ya bajeti
ya mwaka wa fedha 2015/2016, Waziri huyo amesema kuwa Ofisi ya Makamu
wa Rais imekamilisha kanuni mpya ya mifuko ya plastiki zinazorekebisha
viwango vya unene unaoruhusiwa kutoka Maikroni 30 kwenda Maikroni 50.
Waziri Makamba amesema kuwa
kanuni hizo tayari zimesainiwa kupitia tangazo la Serikali Na.271 la
mwaka 2015 na kutolewa katika Gazeti la Serikali Julai 17, 2015 na
kupewa Na. 29.
Kwa upande wake mwanafunzi mwenye
umri wa miaka 16 wa kidato cha tatu anayesoma shule ya Sekondari
Mnarani iliyopo jijini Mwanza Getrude Clement ambaye alihutubia viongozi
mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu
mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani amewahimiza
Watanzania kutunza mazingira na kufauata maelekezo yanayotolewa na
Serikali na wataalamu wa mazingira ili kuyatunza mazingira wanamoishi.
Getrude amesema kuwa amefarikjika
kwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania na dunia kwenye mkutano wa
mabadiliko ya tabia nchi ambapo mataifa 175 yalikutana kusaini
makubaliano ya Paris.
Katika kuwahimiza vijana kujenga
tabia ya kutunza mazingira, Getrde amewaasa vijana hasa wanafunzi
kusimamia sauala la utunzaji wa mazingira wakiwa shuleni kwa kwa
kujiunga na klabu mbalimbali ambapo yeye amejiunga na klabu ya “Mali
Hai” iliyopo shuleni anaposoma.
Kwa upande wa Watanzania kwa
ujumla kwenye utunzaji wa mazingira, Getrude amesema kuwa ni vema
wajifunze kutoka mataifa mengine yanavyosimamia utunzaji wa mazingira
hasa matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mwanafunzi huyo amekaribishwa na
kutambulishwa kwa wabunge leo mjini Dodoma kwa heshima ya kuliwakilisha
vema taifa wakati wa utiaji saini makubaliano ya namna ya kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki
moon alimkaribisha Getrude kwa viongozi hao na kusema “Ni furaha yangu
kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi
Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana”.