Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mwabukoli wilayani Meatu
Mkoani Simiyu, wakifuatilia Hotuba ya Naibu Waziri Mpina (hayupo Pichani)
alipotembelea kijijini hapo, wenyeji hao wa kabila la kisukuma, wapo na vifaa
vyao vya jadi wakifanya dawa kwa utaratibu wa kudumisha mila zao wakati wa
ngoma ya mavuno. EVELYN MKOKOI,MEATU
Wakazi wa kijiji cha
Mwabukoli kilichopo Wilayani Meatu Mkoani Siiyu katika kata ya Kisesa, wamekumbana
na Changamoto za kimazingira kutokana na kile kinachodaiwa ni utekelezaji wa
sheria ya mazingira ya mwaka 2004 kifungu 57 (1) kinachokataza shughuli zozote za
kibinadamu ndani ya mita sitini (60) ya
vyanzo vya maji, mito, maziwa na bahari.
Sheria hiyo ya mazingira imewabana wakazi wa kata ya Kisesa,
Mwabawa,Mwasegela na Lingeka kutokana na kuwakataza wananchi wa kata hizo
wasifanye shughuli zozote za kibinadamu kama vile kufanya kilimo, kuchota maji,
kuchunga na kulisha mifugo, kuchota mchanga, kukusanya kokoto, kuchimba na kuponda mawe.
Katazo hilo la serikali
linatoakana na sababu kuwa maeneo hayo yana ardhi oevu na yenye rutuba na
kutokana na hali ya ukame katika maeneo ya mkoa huyo ardhi hii inaruhu mazao
kustawi vizuzi.
Awali akitolea
ufafanunuzi wa suala zima la uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji, waziri
wa nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira mhe. Luhaga Mpina
alisema kuwa, serkali ya Tanzania ilipata ufadhili kutoka Mfuko wa mazingira wa dunia dunia (GEF), Bank
ya Dunia na shirika la (SIDA) kupitia mradi wa Program ya kuhifadhi mazingira
wa ziwa Victoria ( LVEMP )
Naibu Waziri Mpina, alieleza kuwa awamu ya kwanza ya mradi huo uliokuwa
ukisimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Raisi
kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usumamizi wa Mazingira (NEMC), uliojulikana kama mradi wa kuhifadhi ziwa
Victoria, (LVEMP) uliwataka wananchi kuibua miradi mbadala itakayo wawezesha
wananchi kufanya shunguli mbadala za kiuchumi bila kuharibu mazingira, kama
vile ufugaji nyuki, bustani, ufugaji kuku, samaki na kilimo cha matrekata wangombe
wa kisasa.
Mhe. Mpina
aliwafafanulia wakazi wa kata hizo katika mkutano wake wa hadhara ulofanyika
kijijini Mwabukoli kuwa, awamu ya pili ya mradi huo unahusisha nchi za afrika
mashariki, ambapo hapa nchini kwa sasa suala hilo lipo chini ya wizara ya maji
lakini atachukua jukumu la kuongea na wizara na sector husika ili kuona ni
namana gani wananchi wanaweza kunufaika na mradi huo.
Aidha, akiwasilisha
changamoto hizo diwani wa kata ya kisesa (CCM) mhe. Sasa Kishola alieza kuwa
pamoja na miradi hiyo mbadala kuibuliwa bado haijatoshelesha mahitaji ya wananchi
kiuchumi, hivyo kupitia mkakati huu wa kitaifa wa kupanda miti na
kuhifadhi vyanzo vya maji, serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Raisi iangalie
namna ambavyo wakazi wa kata hizo watakavyoweza kutumia maeno hayo uoevu kupanda
miti ya biashara kama vile miti ya matunda na miti ya mbao ili kuweza kuinua
kipato chao na kukuza uchumi wa nchi bila kuharibu mazngira.
Ziara hiyo ya Naibu WAziri Mpina Wilayani
Meatu mwishoni mwa wiki, ilikuwa na lengo la kushiriki usafi wa mazingira
pamoja na utekelezaji wa mkakati wa kitaifa ya kupanda miti na kuhifadhi vyanzo
vya maji.